AfyaHabariKimataifaMazingiraNewsScience

Viongozi wa Kidini wataka mataifa ya kigeni kufidia mataifa yalioathirika na tabia nchi Afrika.

Viongozi wa kidini wanataka mazungumzu ya mabadiliko ya tabianchi ulimwenguni kujumuisha makundi mbalimbali ili kutafuta suluhu mwafaka wa matatizo hayo.
Viongozi hao kutoka mataifa ya bara Afrika wakiongozaa na Sheikh Ibrahim Lithome kutoka shirika la kimataifa la harakati za uhifadhi wa mazingira la Green Faith Afrika, wamekashifu hatua ya baadhi ya makundi kuachwa nje katika kongamano la ACS linaloendea jijini Nairobi, wakisema makundi hayo huenda yakawa na maono muhimu ya kupambana na tabianchi.
Lithome anasema ingekuwa vyema hata viongozi wa kidini kushirikishwa katika kongamano hilo badala ya viongozi wa kitaifa na siasa pekee.
“Maandamano haya yamefanyika kwasababu Kuna baadhi ya watu wanaona hawajakilishwa pale,Hatuwezi kubadilisha matatizo ikiwa ni viongozi pekeyao,Ni lazima kila mmoja wetu ahusishwe katika jambo hili.” Sheikh Lithome Alisema.


Wakati huohuo Lithome ameyataka mataifa yaliyoendelea na kusababisha uchafuzi wa mazingira kutokana na viwanda vyao, kufidia mataifa ya Afrika yalioathirika na tabia nchi.
“Tunatoa wito Kwa nchi ambazo zimeendelea Kwa sababu uchafuzi mkubwa unatokana na wao, wagharimie uharibifu ambao umetokea katika ulimwengu, na si Kwa mikopo ila wafidie mataifa ya Afrika.” Sheikh Lithome aliongeza.
Shirika la Green Faith Afrika lilikuwa limeleta pamoja viongozi wa dini mbalimbali,kutoka mataifa mbalimbali barani Afrika kujadili masuala ya kutatua mabadiliko ya tabia nchi, sambamba na Kongamano linaloendea la tabianchi Barani Afrika jijini Nairobi.