FoodHabariNews

Shilingi 35m  Zatengwa Kufufua kilimo cha Korosho na Nazi Kilifi

Kilimo cha korosho kimefahamika sana kutokana na mchago wake wa kuimarisha uchumi wa ukanda wa pwani, hii ni kufuatia kuanzishwa kwa kiwanda cha zao hilo mjini Kilifi mnamo mwaka wa 1975. Hata hivyo kilimo cha korosho kimefifia baada ya kusambaratika kwa kiwanda hicho mnamo mwaka 1996.

Mikakati ya kufufua kilimo cha korosho na nazi kaunti ya Kilifi huenda ikazaa matunda, kufuatia mpango wa serikali wa kukuza vyakula vinavyotoa mafuta yanayotumiwa kupikia.

Waziri wa kilimo Mithika Linturi alisema kuwa serikali imeweka kipaumbele kilimo cha mmea wa mkorosho na mnazi kama njia ya kuipunguzia serikali gharama ya uagizaji wa mafuta ya kupikia kutoka nje ya nchi, huku akiwahimiza wakulima kujiandikisha ili kunufaika na miradi ya serikali, ikiwemo  kupokea mbolea ya bei nafuu.

Ni muhimu sana kwa nchi yetu sababu tukiongeza uzalishaji wa mazao yanayotoa mafuta tutapunguza pesa tunazotumia kununua mafuta kutoka huko nje, na pia tukiongea ukulima wa mimea hii nyinyi kina mama mumepata kazi ya kufanya” Alisema

Mbunge wa Kilifi kaskazini Owen Baya ambaye alikuwa ameandamana na waziri huyo wa kilimo alithibitisha kuwa serikali tayari ilitenga shilingi milioni 35 katika bajeti ya kitaifa ili kufufua kilimo cha korosho kaunti ya Kilifi. Baya aliongeza kuwa kilimo cha nazi aidha kilitengewa shilingi milioni 65 katika bajeti ya mwaka 2023.

Kiongozi hyo wa Kilifi alitoa wito kwa serikali kurejesha hadhi ya kaunti ya hio na pwani kwa jumla kwa kuhakikisha kuwa kilimo cha mazao hayo kinaimarishwa, kwa kufufua kiwanda cha korosho mjini Kilifi.

katika bajeti ya mwaka huu wa kitaifa  sababu ni kiongozi pale bunge niliweka pesa ya huu mtambo milioni 35, ya kufufua kilimo cha korosho hapa Kilifi,iyo pesa iko kwa bajeti na iko kwa wizara yako napia nikaweka milioni 65 ya mambo ya nazi” aliongezea Baya

Hayo yalijiri wakati wa ziara ya Linturi kwenye majengo ya kiwanda hicho kilichokuwa na wafanyakazi takriban 6,000 mjini Kilifi kabla ya kusambaratika kwake.

BY ERICKSON KADZEHA