HabariNews

HALI HALISI! Uraibu wa Pombe wapita Mipaka nchini Kenya

Tafiti zilizofanywa na halmashauri ya kudhibidi dawa na pombe NACADA, zimebaini kuwa pombe ndio kileo kinachotumika vibaya nchini Kenya.

Tafiti hii ya kitaifa mwaka 2022 zilonyesha kuwa Mmoja kati ya wakenya 8 wenye umri wa miaka 15 – 65 ni mraibu wa pombe , hii ikichangia idadi ya watu 3,199,119 kuathirika na uraibu wa kileo hicho.

Maeneo ya magharibi mwa Kenya kuliripotiwa kuenea zaidi kwa unywaji wa pombe kwa 23.8% ikifuatiwa na mwambao wa pwani kwa 13.9% na mkoa wa kati ukienea kwa 12.8%.

Nairobi Aidha , ilibainika kuenea zaidi kwa watengenezaji wa pombe halali kwa 10.3%, mkoa wa Kati wakienea kwa 10.0% na mkoa wa Mashariki wakiwa 8.4%.

Kwa upande mwingine utumiziwa chang’aa uliripotiwa kuongezeka kwa 12.9% katika mkoa wa Magharibi, Nyanza ikifuata katika nafasi ya pili kwa 6.3% huku Rift Valley ikienea kwa 3.6%.

Utumizi mkubwa wa pombe za kitamaduni vile vile uliripotiwa katika mkoa wa Magharibi kwa 12.9% ikifuatiwa na mkoa wa Pwani na Nyanza kwa 7.4% na 2.2% mtawalia .

Vileo vilivyo rahisi kubeba maarufu ‘spirits’ havikusahaulika, vileo hivi viliripotiwa kutumika kwa hali ya juu zaidi katika mkoa wa Kati kwa 4.1% , Pwani ikiwa na 3.2% ikimaliziwa na Rift Valley kwa 3.1%.

Hata hivyo utafiti zaidi ubanisha Umri wa wastani ya waraibu wa Pombe, Tumbaku, miraa, bhangi, cocaine, heroin pamoja na dawa nyinginezo ni kati ya umri wa miaka 16 – 20.

BY EDITORIAL DESK