HabariNews

Bilioni 1 zatengwa kwa Uzinduzi waVitambulisho vya Kidijitali

Serikali imetenga shilingi bilioni 1 kufanikisha mradi wa usajili wa vitambulisho vipya vya kidijitali, UPIs.

Kulingana na Katibu wa Idara ya Uhamiaji nchini Julius Bitoke kitambulisho hicho kitapeanwa kwa wakenya wote wanapozaliwa.

Bitoke alibaini kuwa kitambulisho hicho kitatumika rasmi katika nyanja zote za elimu, ulipaji ushuru kupitia KRA na pia kitatumika kama nambari ya cheti cha kufariki pindi mmiliki atakapoaga dunia.

“Nadhani huu ni muda mwafaka katika taifa hili kuzungumzia utoaji vitambulisho vya kidigitali ni muhimu na ni vizuri kukumbatia mradi huu ili tuwezesha kusongesha taifa mbele.” Alisema Bitoke.

Bitoke Aidha alisema kuwa Wakenya ambao watafikisha umri wa miaka 18 watapewa kadi ya utambulisho itakayoitwa Maisha Card.

“Tutakuwa sasa na nambari mpya itakayoitwa Maisha Number ambayo kila mtu anayezaliwa Kenya atakuwa nayo. Itakuwa ni nambari ya kuzaliwa, inayotumika kwenye Kitambulisho cha Kitaifa, katika kazi, kwa KRA,” alisema Bitok.

Kitambulisho hicho kinachotarajiwa kuzinduliwa tarehe 29 mwezi huu kitatoa maelezo ya wakenya kwenye kadi huku kikitoa utumizi wa kitambulisho kinachotumika kwa sasa.

BY MJOMBA RASHID