HabariNews

Kaunti ya Kilifi yawekeza zaidi kwenye vyuo vya kiufundi Kuvutia Vijana katika Elimu

Serikali ya kaunti ya Kilifi inapania kuwekeza zaidi kwenye sekta ya elimu ya vyuo vya kiufundi ili kukabiliana na tatizo la ukosefu wa ajira miongoni mwa vijana.

Ulegevu wa wakaazi  kujiunga na vyuo vya kiufundi kaunti ya Kilifi imeisababisha serikali ya kaunti ya hio kuweka mikakati mipya ili kuvutia wanafunzi zaidi.

Kulingana na Waziri wa elimu kaunti ya Kilifi Felkin Kaingu, ukosefu wa wanafunzi kwenye taasisi hizo umetokana na ulegevu wa kufuatilia shughuli za masomo jinsi zinavyoendelea.

Kaingu alisema kuwa serikali ya kaunti hio imewekeza zaidi kwenye vyuo hivyo ili kuboresha viwango vya elimu vinatolewa  pamoja na kuvutia wanafunzi zaidi.

Mtu anapoenda shule huwa ana matazamio, je hii matazamio yake atayawezesha baadaye? Hii ndio kitu tunajaribu kuangalia saii, vijana wetu wako na ari wako na akili za kutaka kusoma lakini tumekuwa hatujawekea mkazo katika hizi vyu. Tunataka tubadilishe niya zetu tuhakikishe kwamba  tumewekeza katika hivi vyuo.” Alisema.

Kaingu hata hivyo alisisitiza kuwa idara yake itaweka data za majina ya wanafunzi waliosomea kwenye vyuo vya kiufundi vya serikali ili kuwasaidia kutafuta kazi kupitia kampuni na washirika wa ndani serikalini  pamoja na wa nje ya nchi.

tuko pia na kampeni ya kuleta washikadau zaidi katika kazi hii, tunataka tuwe na mashiko mpaka nje ya kaunti hii , nje ya nchi ili vijana wetu wanapo maliza katika hizi vyuo wawetutawatafutia kazi. Tunataka tutengeze hazina na data ya wale vijana wote ambao watamaliza katika VTCs ili tuwasiliane nao tuwasaidie kutafuta kazi.” Aliongezea Kaingu

BY ERICKSON KADZEHA