HabariLifestyleNews

Kamati ya Mazungumzo ya Maridhiano yalilia Fedha Kufadhili mazungumzo hayo

Kamati ya mazungumzo ya maridhiano kati ya serikali na upinzani sasa inataka fedha za kufadhili vikao vyao.

Taarifa za ndani zimearifu kuwa Kamati hiyo ambayo Jumatano Septemba 13 ilifanya mazungumzo na Spika wa Bunge la Kitaifa Moses Wetangula inataka fedha kufadhili mazungumzo hayo.

Kinara wa Kenya Kwanza kwenye mazungumzo hayo Kimani Ichungwa na mwenzake wa Azimio Kalonzo Musyoka walifika bungeni mapema siku ya Jumatano.

Inaarifiwa kuwa ukosefu wa fedha umesababisha kucheleweshwa kwa shughuli zao. 

Mkutano huo na Spika Wetangula umedumu kwa takribani saa moja aidha ulihudhuriwa na wanakamati wa pande zote akiwemo Kiongozi wa wachache bunge la Kitaifa Opiyo Wandayi na Mbunge wa EALA Hassan Omar Sarai.

Duru za habari, kamati hiyo ya mazungumzo ya maridhiano imekuwa na wasiwasi kuhusu ukosefu wa ufadhili wa fedha kuwawezesha kukamilisha jukumu waliloweka na hivyo basi kuchelewesha shughuli zao.

Kulingana na vyanzo hivyo vya taarifa Kamati hiyo ilitaka kukutana na Spika kumuomba kutenga bajeti maalum ya kamati hiyo, ikikumbukwa kuwa vikao hivyo vilipangwa kufanywa kwa muda wa siku 60 na wiki mbili zimepita bila mafanikio yoyote.

Hata hivyo haijabainika ni kima gani cha fedha kitakachotengwa na kumgharimu mwananchi zaidi.

NA Mjomba Rashid