Kamati ya afya katika bunge la seneti imeanzisha juhudi za kujumuisha serikali za kaunti kuhusu bima mpya ya afya ikidokeza kuwa miswada kadhaa iliwasilishwa katika bunge la kitaifa ili kuwe na mfumo mmoja wa utoaji huduma wa bima ya afya.
Katibu Mkuu wa kamati ya afya katika bunge la seneti Harry Kimtai, imeeleza juhudi za kamati hiyo kujumuisha serikali za kaunti kuhusu bima mpya ya afya huku akidokeza kuwa miswada kadhaa iliwasilishwa katika bunge ya kitaifa ili kuwe na mfumo mmoja wa utoaji huduma wa bima ya afya.
Kulingana na mkuu wa kamati hio Harry Kimtai, hatua hiyo itawezesha kila mkenya kulipia bima ya afya ili kupata huduma za afya bila matatizo yoyote huku akisisitiza hatua hiyo itawezesha hata wale walio na mapato ya chini kupata huduma hiyo.
“Kila nyumba lazima isajiliwe kwa bima ya afya ili jamii isaidike kwa huduma bora za kiafya,na kuna manufaa kama vile Primay Health Care Fund ambapo itashughulikia hospitali za chini, Social Health Care itashughulikia boma na Emergency Critical and illness ambapo itabidia watu wenyee magonjwa sugu ili wasiumize tena jamii na familia wakati ni wagonjwa lakini kila mtu ajisajili kwa huu mfumo mpya,” asema Kimtai.
Hatua hiyo iliungwa mkono na mwenyekiti wa kamati hiyo Jackson Madango ambaye alitaja mpango wa NHIF kuwezesha serikali kua na mfumo mmoja wa kulipia bima ya afya
Mandago Vile vile alisisitiza kuwa hakuna Mkenya atakayewezwa kutozwa bima ya afya mara mbili huju wakiitaka huduma hiyo iwe chini ya usimamizi wa UHC.
“Mswada huu mpya unaenda kubadili ile NHIF ya zamani sasa utajiunga na huu mpya,haimanishi kwamba utakatwa pesa mara mbili hapana utakatwa mara moja”,asema Mandago.
Kwa upande wake Harry alitoa onyo kwa yeyote atakayechelewa kulipa bima hiyo atatozwa faini.
“Tukigundua haujalipa na unataka matibabu lazima ulipe kwanza faini ndio upate huduma za afya”,aeleza HarryB