GamingHabariMichezoNewsSports

Kenya Shujaa Wapokea donge la sh 3m kwa Kuinyuka Afrika Kusini

Timu  ya raga ya wachezaji saba nchini Kenya Shujaa wametunukiwa kiima cha sh 3 milioni kutokana na juhuzi za kunyakua kombe la raga Afrika la wachwzaji saba kila upande.

Wana shujaa chini ya ukufunzi wa kocha Kelvin ‘Bling’ Wambua, waliregae nchini kutoka Harare, Zimbabwe Septemba 17 baada ya kuinyuka Afrika kusini 17-12 katika kinyang’anyiro cha kuvhukua ubingwa wa raga Afrika. Kuwasili kwao katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta (JKIA) jijini Nairobi kulipokelewa na vifij na nderemo kutoka kwa mashabiki waliosimamisha shughuli katika uwanja huo.

PICHA / HISANI

Mapema Jumanne, Waziri wa Michezo Ababu Namwamba amekutana na kikosi hicho kilichojumuisha wachezaji sita wapya na sita wazoefu pamoja na maafisa wake wakiongozwa na Wambua na viongozi wa Shirikisho la Raga Kenya (KRU) akiwemo mwenyekiti Sasha Mutai.

“Huwa hatuzitunuku timu zikishiriki mashindano ya kuingia Olimpiki, lakini kwa sababu mlifanya makubwa kwa kuangusha timu zote wakiwemo miamba Afrika Kusini katika fainali, Rais William Ruto ameahidi mpokee zawadi ya Sh3 milioni,” alisema Ababu

Waziri huyo aidha alitoa hundi kwa timu hiyo katika dhifa ya chakula cha asubuhi iliyogharimiwa na wizara hiyo katika hoteli ya kifahari ya Weston jijini Nairobi.

Ababu alisema kuwa kila mchezaji aliyekuwa Harare atatia mfukoni kitita cha Sh200,000 huku  maafisa sita wa benchi ya kiufundi watapata Sh100,000 kila mmoja.

BY EDITORIAL DESK