HabariNewsWorld

Ukrain Kujenga Bohari la nafaka KPA Mombasa Kumaliza makali ya Njaa Afrika Mashariki

Serikali ya Ukraine imeeleza nia ya kujenga bohari la nafaka nchini Kenya katika mamlaka ya bandari ya Mombasa KPA.

Bohari hilo litatumika katika usafirishaji wa nafaka kama njia moja ya kukabili uhaba wa chakula afrika mashariki. Hii ni baada ya Rais Wa Ukraine Volodymyr Zelensky kumualika rasmi Rais William Ruto kuzuru taifa hilo la Ukraine.

Wawili hao walikutana ana kwa ana baada ya kuamilika kwa mkutano wa wanachama wa umoja wa mataifa huku wote wakieleza kuwa kuna baadhi ya maswala ambayo yanastahili kujadiliwa baina yao.

Rais Ruto hata hivyo, alimpongeza Zelensky kwa kusalia mkakamavu licha ya mazingira ya vita anayokumbana nayo huku akisistiza msimamo wake ni wa kufuatwa kwa sheria na utaratibu kuhusu jambo lolote lile.

BY EDITORIAL DESK