HabariNews

Siku ya Kimataifa ya Amani: Uzinduzi wa Bridgebot kuimarisha maelewano katika mitandao ya Kijamii, yasema SFCG

Na huku ulimwengu ukiadhimisha siku ya Kimataifa ya Amani, harakati zinazendelezwa kuimarisha na kuendeleza uwiano na utangamano katika jamii.

Shirika la Search for Common Ground limezindua mtandao wa mazungumzo ya pamoja katika mtandao wa kijamii, mtandao uitwao Bridgebot.

Judy Kimamo ambaye ni Mkurugenzi wa Shirika la Search nchini Kenya na Somalia kupitia taarifa kwa vyombo vya habari siku ya Alhamisi alisema, Mtandao huo mpya wa BridgeBot, utasaidia watumizi wa mitandao ya kijamii kuzika tofauti zao na kujenga uaminifu na maelewano mtandaoni.

Dunia ikiadhimisha Siku ya Kimataifa ya Amani, SFCG inaadhimisha hatua kubwa muhimu iliyopiga katia, Search imetumia zana za Kidijitali kujenga uaminifu na ushirikiano na leo tuna furaha kuzindua kifaa cha kidijitali kwa jina ‘Bridgebot’ kifaa hiki kipya cha mazungumzo kitasaidia watumizi wa mtandao kuondoa mwanya wa tofaut, kuleta uaminifu na ushirikiano,” alisema.

Kimamo alibaini kuwa uzinduzi wa mtandao huo umejiri baada ya utafiti kuonyesha kuwa asilimia kubwa ya watu hukwepa mijadala mitandaoni inapopamba moto pindi maswala mbali mbali yanapoibuka.

Aidha alisema ni asilimia chache ya watu huwa huru ya kutoa maoni yao huku wengine wakihisi kuwa wabunifu mitandaoni.

SFCG iliunda Bridgebot pamoja na AI baada ya utafiti kunyesha kuwa wengi hukwepa mazungumzo wanapohisi kulemewa na mijadala inapopamba moto na aidha pindi wanapohisi kuwa walengwa wa mijadala hiyo.”

Utaifti aidha umeonyesha kuwa wachache wako sawa kutumia fursa hii na kupata suluhu watakapotumia mtandao wa Bridgebot,” aliongeza Bi. Kimamo.

Aidha Kimamo kuwa BridgeBot itasaidia watumiaji wa mitandao ya kijamii kufikiria tofauti kwa kuwapa ujuzi na mitazamo, utambulisho, kufanya mawasilisnao yasiyo na viurugu.

Pia Kimamo amesema uzinduzi huo utafanyika katika katika baadhi ya nchi zilizoathiriwa zaidi na migogoro ya kimawasiliano kwa ushirikiano na wanateknolojia, watafiti, wasomi, mashirika yanayoongozwa na vijana na ili kuapusha hali ya mogogoro kwa kutumia uzinduzi huo ambao kufikia sasa umafanyiwa majaribio ya miezi 7 na kuthibitiwa kufanya kazi.

Mtandao huo ulishazinduliwa katika mataifa ya Sri Lanka, Nigeria na hapa nchini Kenya na hivi karibuni utazinduliwa huko Jordan na Lebanon.

Kwa mtu kutumia mtandao huo wa bot atahitajika kutembelea tuvuti https://www.sfcg.org/bridgebot/.

BY MJOMBA RASHID