HabariNews

KEMNAC yapinga Ubnafsishwaji wa bandari ya Mombasa KPA

Baraza la kitaifa la Ushauri wa dini ya kiislamu nchini Kenya KEMNAC limelaani  vikali pendekezo la kutaka sehemu ya mamlaka ya bandari ya Mombasa KPA kubinafsishwa na serikali.

Mwenyekiti wa baraza hilo Juma Ngao alisema iwapo serikali ina nia ya kuboresha bandari ya Mombasa ianze na sekta ya majani chai akisema kuwa pendekezo hilo halikuhusisha maoni ya wananchi hali ambayo wameitataja kuwa kinyume cha sheria.

Ngao aidha aliwarai wabunge wote hususan wa Pwani kusimama kidete katika kupinga pendekezo hilo akisema kila mkoa humu nchini umebarikiwa na raslimali zake.

Kama mnataka kuuza bandari ya Mombasa kwamaba ndio mbinu ya kufanya maendeleo kwanza anzeni kubinafsisha sekta ya kahawa na majani chai.”alisema Ngao.

Wakati huo huo Ngao aliukosoa uongozi wa rais William Ruto kwa kutotimiza ahadi alizoahidi wakati wa kampeni ikiwemo kushusha gharama ya maisha.

Chini ya utawala huu wa Kenya Kwanza hatuko  salama kwanza walishindwa kupunguza unga kwa siku 100 iliwashinda sasa sisi tunauliza kama viongozi wa dini kwani mahidi kukauka ni miezi mingapi?” Aliuliza Ngao.

Kwa upande wake Naibu mwenyekiti wa baraza hilo Abubakar Amin alipongeza hatua ya gavana wa kaunti ya Mombasa Abdulswamad Sharrif Nassir kwa kuwa msitari wa mbele kupinga pendekezo hilo akisema kauli yake imeashiria maslahi ya Wapwani akiwarai viongozi wengine kusimama naye katika kupigania haki ya Mpwani.

Aliyozungumza Gavana Nassir ni kwamba hatakubali na twaomba viongozi wote kusimama naye maana hii ndio kitenga uchumi chetu sisi wapwani ikiwa bandari kuu haitakauwa salama basi tungojeni kuwa waombaji vibarua leo kipo kesho hakuna.”Alisema Amin.

Na Medza Mdoe.