HabariNews

NAFUU kwa Jalang’o na Tom Ojienda Mahakama ikisongeza mbele Kufurushwa kwao

Mahakama ya kutatua Mizozo ya Vyama vya Kisiasa imeongeza muda Kwa agizo la kuwatimua Seneta wa Kisumu Tom Ojienda na wabunge Phelix Odiwuor almaarufu Jalang’o na Elisha Odhiambo kutoka kwa chama cha ODM.

Mwenyekiti wa baraza hilo Dezma Nungo amekitaka chama cha ODM pamoja na ofisi ya msajili wa vyama vya kisiasa kutoa mwelekeo kuhusu suala hilo. Kesi hiyo itatajwa Oktoba tarehe tatu mwaka huu.

“Katika muda unaosubiri kusikilizwa na kuamuliwa kwa Ombi hili, Baraza hili Tukufu linatoa maagizo ya muda ya kusimamisha utekelezaji na/au utekelezaji wa uamuzi wa Mlalamikiwa wa Kwanza wa kumfukuza Mlalamishi/Waombaji, kutoka kwa Chama cha Orange Democratic Movement, ” Desma alisema kwenye karatasi za mahakama.

Uamuzi kutoka kwa baraza hilo unajiri baada ya wawili hao pamoja na  mbunge wa Lang’ata Felix Oduor – Jalang’o kuwasilisha kesi wakipinga hatua ya ODM kuwaadhibu.

Wanahoji kuwa mnamo Septemba 6, 2023,walishangazwa kwa kutosikilizwa kutokana na maai yanayowakabilihuku huku chama cha ODM kikipitisha mapendekezo ya Kamati ya Nidhamu ya ODM kuwafurusha chamani na kufuta usajili wa wanachama hao.

Uamuzi kuhusu ombi la jalang’o hata hivyo unatarajiwa kutolewa Jumatatu 25, Septemba.

BY EDITORIAL DESK