HabariNews

Mwanaharakati Ogolla Apinga kuongezwa muda wa kuhudumu kwa rais Nchini Kenya

Mwanaharakati wa maswala ya utawala Fred Ogolla amepinga pendekezo la seneta wa Nandi Samson Cherarigei la kutaka muda wa kuhudumu kwa rais kuongezwa kutoka miaka 5 hadi 7.

Pendekezo hilo limekuja wakati ambapo Wakenya wanalilia gharama ya juu ya maisha, bei ya juu ya mafuta ikiwa kidonda uchungu kwa taifa na sekta mbali mbali nchini.

Kulingana na Ogola pendekezo hilo halifai kutolewa kwa umma kutokana na dhiki zinazowakumba wananchi akisema kuwa raiaa wanapaswa kupewa kipaumblele katika maswala yanayowaathiri ikiwemo kushusha gharama ya maisha.

“Iyo imekuja kwa wakati mbaya wakati wakenya wanasumbuka na gharama ya maisha watu wanalala njaa watu wanakosa mahala pa kulala pesa ya kwenda kufanya matibabu hakuna  elimu, kila kitu kuna shida nyingi sana za kiuchumi, wakenya hawajapendekeza mambo ya kuongeza muhula kwa rais mbona imetoka kwao watu huwa wanaongezwa muda wa kuhudumu kulingana nay ale wametenda how have this government perfom ili watuulize ya kuwa wanataka waongezwe muda” alisema

Mazungumzo yanayoendelea ya maridhano aidha Ogolla ameyataja kama kizuizi na badiliyake akiwataka kuangazia masuala na maslahi ya mwananchi.

“Kama wangekuwa BOMAS kujaribu kuangalia vile wanaweza kutatua mambo ya uchumi iyo ni suala muhimu ambayo wakenya wangesikiza badala ya kusikiza mambo ya term. Kuna vile vipengele ambaozo zingefaa ziangaliwe kwa kina zaidi wakati wa hayo mazungumzo ya maridhiano, lakini tukaanza kusikia kama mambo imeshift ya muhula kwa kuhudumu kwa rais tunakua na wasiwasi mno kwa sababu ni kama walikuwa wanatudanganya ili waanze mambo ya kubadilisha katiba na kuanza kuweka vitu zingine ambozo sio vitu wakenya walistahili”

Kauli yake imejiri baada ya chama cha cha UDA kujitenga na hoja ya seneta huyo kikisema hakina nia ya kuenda kinyume na muhula iliyowekwa katika katiba badala yake kinajizatiti kutimiza ahadi walizotoa wakati wa kampeni pamoja na kujipanga kwa siasa za mwaka 2027.

BY EDITORIAL DESK