HabariNews

Wakaazi watakiwa kushiriki Mchezo wa Ludo Kukuza Amani

Wakaazi wa Mombasa wamehimizwa kutumia michezo mbalimbali ikiwemo ludo badala ya mchezo wa mpira pekee katika kuhamasishaji wa amani na utengamano miongoni mwa jamii.

Kulingana na Mwelekezi mkuu katika shirika la Amkeni Community Organization Christine Kaguya, mchezo huo utaleta uwiano na kuondoa hofu miongoni mwa jamii na vyombo vya usalama.

Aidha Kaguya alisema kuwa amani ndio nguzo muhimu katika ukuaji wa taifa akidokeza kuwa wameshirikisha na washikadau mbalimbali ili kusambaza amani kupitia mchezo huo.

“Tumekuja na njia tofauti zitakazoleta vijana pamoja, tumegundua na kuona ni vipi maskai zinazocheza Ludo tutaziwekeza vipi ili kutumika kama ala ya kuambaza amani isiwe mpira pekee.” Alisema Kaguya

Kwa upande wake mwenyekiti wa balozi la amani katika kata ndogo ya kadzandani eneo bunge la Nyali (DPC) Cornelius Odhiambo, hatua hiyo aliitaja kuwa ya muhimu kwani itatoa vijana wengi katika lindi la mihadarati

Odhiambo aidha aliongezea kuwa uhalifu umepungua kwa asilimia kubwa kwa kushirikiana na washika dau mbalimbali kutoa hamasa la amani kwa jamii.

“Amani haiwezi kuelekezwa na mtu mmoja tu na tunataka amani iwe kielelezo katika Mombasa nzima ,pia  tunafurahia kusikia kwamba hali ya utovu wa nidhamu imerudi chini sana na watu wanapenda amani.” Alisema Odhiambo

BY EDITORIAL DESK