HabariNews

Matamshi ya Naibu rais Rigathi SI ya Uchochezi asema Karisa Nzai

Mshauri wa maswala ya kisiasa katika afisa ya rais nchini karisa nzaia amepinga madai kuwa matamshi ya naibu wa rais Rigathi Gachagua kuhusu taifa la kenya kuongozwa kikampuni ni ya ubaguzi, akisema kuwa kauli hiyo inaashiria kuwa utawala wa rais ruto utaangazia viongozi ambao wanakumbatia mfumo wa utawala wake i bali sio kubagua jamii ambazo hazikuunga mkono kenya kwanza wakati wa uchaguzi.

Akizunguma na sauti ya pani kwenye kipindi cha Baraza letu Nzai alisema kuwa wapinzani ni vyombo vya habari wanatafsiri kauli hiyo kinyume na maaana yake kwani Gachagua anapigia upate viongozi walionauweledi wa utawala wa rais wiliam ruto .

“Mna maanisha kivingine kike alichokisema Ni kuwa huwezi kuweka MTU ambae alikuwa anapinga maono yako Na kuendelea ajenda zako serikali huyo MTU si atakumaliza ? Sasa wewe hukusaidia rais katika mipango yake Na unataka akuweke mshauri si utamshauri kivingine udidimie. Kimaendeleo rais anazingatia kila eneo ” alisema Nzai.

Nzai alisema haya muda mchache baada ya Naibu wa rais Rigadhi Gachagua kushikili kuwa utawala wa kenya kwanza unakumbatia mfumo wa kikampuni.
Kiongozi huyo wa chache wa zamani katika bunge la kaunti ya Mombasa aidha aliwashauri wandani wa chama cha UDA kujitoa kimasomaso katika kuwania nyadhafa mbali mbali za chama hicho kwenye uchagauzi unaotarajiwa kufanyika decemba 9 mwaka huu.
Nzai amesisitiza kuwa uchaguzi huo utakuwa wa uhuru na wazi .

“Sasa tunataka kuwa Na uchaguzi kutoka desemba tarehe tisa mtunyeyote ambae anataka kuwania kiti kutoka kule poling station mashinani mpaka kaunti basi ako Na uhuru Na hii tulifanya maonyesho Jana hakuna kitu cha kujificha ficha Kuna uwazi Na uhuru katika uchaguzi hakuna mwenye atachukuliwa Kwa kuwa anajuana Na rais Na tumeweka teknolojia YA kisasa kuhakisha kuwa hakuna wizi Wa Kura”

Kiongozi huyo kadhalika amewataka wafuasi wa baadhi ya viongozi kutoka kaunti ya Mombasa kuendeleza ushirikiana kabla na hata baada ya uchaguzi kwani chama cha UDA kinahitaji nguvu zaidi.
” Na Hawa viongozi wote nishazungumza nao , nishaongea Hassani nimeongea Na Mohammed Ali Na tumeongea kama viongozi tukasema sasa hili joto la kisiasa tutalimaza tarehe tisa desemba kwenye uchaguzi Wa chama Kisha bado Sisi tuanahitaji bado kupendana Na hao wanounga mkono mohamed Ali Na Sarai wote Ni wa chama” aliongeza bwana Nzai