AfyaHabariLifestyleMombasa

Rais William Ruto amepinga madai yanayoendelea kuhusiana na ubinafsishaji wa bandari ya Mombasa

Rais William Ruto amepinga madai yanayoendelea kuhusiana na ubinafsishaji wa bandari ya Mombasa kwamba hakuna yeyote atakayebinafsisha bandari hiyo.

Akizumgumza katika mkutano wa chama cha UDA kwenye ukumbi wa Bomas Jijini Nairobi tarehe 29 mwezi wa septemba mwaka huu, Rais Ruto alidokeza kwamba serikali ya Kenya kwanza iko na mikakati ya kufanya upanuzi wa bandari hiyo ili kuvutia wawekezaji wengi zaidi kutoka sehemu mbalibali ulimwenguni

Rais Ruto alirejelea kauli yake katika uwanja wa Kasarani wakati wa kula kiapo kulitumkia taifa mnamo tarehe 15 Septemba 2022 aliyekariri kwamba huduma za bandari ya Mombasa lazima zirejeshwe kikamilifu ili kunufaisha wakaazi wa Mombasa na wapwani kwa ujumla.

“Mambo ya ubinasfishaji bandari ya Mombasa haitafanyika kwa serikali yangu, yale mambo ambayo tunataka kufanya kama serikali ni upanuzi wa bandari hiyo ili kuvutia watu mbalimbali ili kutengeneza ajira na hivyo ndivyo nilivyosema tangu siku ya kwanza wa kula kiapo.” Alisema rais Ruto.

Wakati huo huo kiongozi wa taifa alidokeza kuwa serikali inalenga kutia saini miswada yote inayohusiana na afya kabla ya mwisho wa mwezi ujao.

Rais Ruto alisema miswada hiyo itasaidia kuupisha mpango mkuu wa serikali ya Kenya Kwanza wa utekekelezaji wa afya kwa wote.

“Nataka kuwashukuru wabunge kwa kufanya kazi nzuri na niko tayari kuweka sahihi sheria zote sababu nilipewa ripoti kuhusiana na miswada ya sheria iliyokuwa bungeni iko tayari kufanyiwa tathmini zaidi na hii itasaidia sana mambo ya afya kwa wote tuwe na mfumo mzuri kwa afya kwa wote”…….alisisitiza Rais Ruto.

 

BY NEWS DESK