HabariNews

Paspoti 15,400 Zipo tayari Kuchukuliwa wiki hii, Asema Kindiki

Paspoti 15,400 ziko tayari kuchukuliwa katika vituo tofauti vya uhamiaji wiki hii. Haya ni kwa mujibu wa waziri wa ndani Prof. Kithure Kindiki.

Hatua hii inajiri baada ya kukusanywa kwa paspoti 22,353 jijini Nairobi na afisi nyingine za uhamiaji katika kanda zote nchini Kenya kufuatia kuzinduliwa   kwa mpango wa wa haraka wa utowaji wa paspoti kwa wakenya ‘Rapid Results Initiative’ (RRI).

Kulingana na waziri Kindiki pasipoti zinazostahili zitachukuliwa kutoka Nairobi na afisi zingine ni kama zifuatavyo.

Jijini Nairobi, paspoti 7,501 ziko tayari, 1,166 Mombasa, 1,602 Kisumu na pasipoti 1000 zitachukuliwa mjini Nakuru huku Ofisi nyingine za kanda ambapo pasipoti zitachukuliwa ni Eldoret (1,543), Kisii (1,500) pamoja na Embu (1,088).

“Serikali itaendelea kuoanisha taratibu na mazingira yetu ya utoaji huduma ili kuhakikisha tunaleta ufanisi wa kudumu katika idara ya uhamiaji na kuendeleza vita dhidi ya rushwa ili kurejesha imani ya wananchi,” alisema Kindiki.

Huwenda hii ikasuluhisha baadhi ya malalamiko ya umma kuhusu kucheleweshwa kwa pasi hizo kutokana na ufisadi jambo lililobainika baada ya waziri Kindiki kuzuru jumba la Nyayo ambako ndio makao makuu ya idara ya Uhamiaji.

Wakenya wengi walikashifu ucheleweshaji huo kwa madai ya kukosa nafasi za kazi na usafiri.

Kindiki hata hivyo anatarajiwa kuharakisha shughuli ya uchapishaji wa paspoti hizo.

BY EDITORIAL DESK