HabariNews

Usajili Bila ya Hongo kwa Makurutu, Vinara wa Usalama Waahidi

Maafisa wa usalama wameonywa dhidhi ya kuchukua hongo katika zoezi la usajili wa makurutu linalotarajiwa kuanza humu nchini.

Mweneyekiti wa tume ya huduma kwa polisi Eliudi Kinuthia alionya kuwa hatua kali zitachukuliwa kwa watakaokosa nidhamu. Kinuthia akidokeza kuwa tume hiyo imeweka mikakati dhabiti kukabili visa vyovyote vya ufisadi vitakavyojitokeza wakati wa zoezi hilo.

“Hawa maafisa ambao tutatuma kwenda kufanya usajili, mimi kama muajiri wao akipatikana ofisa yeyote ama mwananchi yeyote, ambaye ameigia kwa kosa la ufisadi wakati wa usajili sisi kama tume tutamchukulia hatua ya kinidhamu na inspekta jenerali anajua tumekubalia hili,” alisema.

Mwenyekiti huyo alisema kuwa tume yake itashirikiana kwa karibu na afisi ya inspekta jenerali Japhet Koome, ili kuhakikisha zoezi hilo linaendeshwa kwa usawa na uwazi.

“ mimi nahakikishia mhesimiwa katika usajili wa maafisa wa polisi, tutafanya kazi kwa pamoja na inspekta jenerali na tutahakikisha ya kwamba wananchi wote ambao wanastahili kupata hii nafasi wamepata kutoka kwa serikali bila ya malipo yoyote,” aliongezea Kinuthia.

Kauli yake imeungwa mkono na Mkurugenzi wa tume hiyo Peter Leley akisema kuwa watahakikisha hakuna visa vyovyote vya ufisadi vitakavyoshuhudiwa wakati wa zoezi hilo.

“kuandikwa kwa askari safari hii itakuwa bila bila ufisadi wa aina yoyote, tuko tayari, amri ya rais imetufikia, tumeweka mikakati, sera tushasajili tayari kazi yetu tuaenda wakati huu tunaambia raia watusaidie waachane na mambo hiyo ya ufisadi,” alisema Leley.

BY EDITORIAL DESK