HabariNews

Seneta Mteula Shakila, Aghadhabishwa na Viongozi wanaoeneza Chuki Lamu

Seneta mteula WA kaunti ya lamu ambae pia ni katibu mkuu wa chama cha Wiper Shakilla Abdallah, ametoa wito kwa serikali kuu na ile ya kaunti kuleta mpango wa hamasa ya amani katika kaunti hiyo ili kuimarisha amani miongoni mwa jamii zinazoisha eneo hilo.

Abdallah akizungumza na Sauti ya Pwani katika kipindi cha gumzo pevu, alisema kuwa kaunti hiyo inahitaji hamasa kuhusu amani ili kuhubiri undugu na umoja ikizingatiwa kuwa eneo hilo limekubwa na ukosefu wa usalama kwa muda sasa.

Nataka kuiomba serikali ituwekee mikakati ama ituletee program ya peace initiative katika jimbo letu la Lamu. Tuweze kuingia chini mashinani kuhubiri amani, upendo na umoja na kushikanisha watu ili tuondoshe tafauti yoyote ilioko.”

Kiongozi huyo Kadhalika aliwataka viongozi wanaotumia nyadhifa zao kueneza chuki miongoni mwa wakaazii kukoma kwani hatua hiyo huwenda  ikazorotesha zaidi usalama.

Shakila alighadhabishwa na hatua ya baadhi ya viongozi kueneza taarifa zinazoamika kuleta mgawanyiko miongoni wa jamii zinazoishi lamu na kutaka serikali kuingilia kati na kuchukuwa  hatua kali za kisheria

Maneno ya watu kutamka maneno ambayo ni ya kuleta mtafaruku baina ya makabila fulani, hio tumeikanya na tumesema hatutaki kuwe na kitu kama hicho. Kitu kilichobaki ni serikali ichukue hatua, mtu  kama amekosea na amekanywa na bado anaendelea kufanya ile kitu serikali inahaki ya kumuita, ” Alisema

Kwa upande mwingine Kuhusiana na mapendekezo ya serikali ya kenya kupeleka maafisa wa polisi Haiti kulinda usalama , seneta huyo alisema kuwa juhudi hizo hazifai kwa sasa kwani taifa la kenya bado linakubwa na lindi la mashamubilizi ya mara mara hasa eneo la lamu .

Shakila hatahiyo alimtaka rais ruto kwanza, afanikisha usalama nyumbani kabla ya kutoa msaada katika mataifa ya nje.

Kwa mtazamo wangu kamaShakila siungi mkono hilo jambo kwa sababu sisi wenyewe tuko na changamoto zetu za kiusalama hapa nchini, na kuna umuhimu kwanza tutatue hizi changamoto zetu tutatue shida zetu, kwanini ikiwa tuko na uwezo wa kuweza kusaidia nchi za njue kwanza tusitatue haya yetu hapa nyumbani,”

Ikumbuwe kuwa mahakama aidha alipiga breki uamuzi wa kuwapeleka maafisa hao Haiti baada ya kesi kuwasilishwa mahakamani kupinga uamuzi huo .

BY DAVID OTIENO