HabariNews

Wakenya Vumilieni! Ongezeko la Bei ya Mafuta lipo nje ya uwezo wa Serikali

Wakenya wametakiwa kuwa wavumilivu kuhusu gharama ya juu ya mafuta, serikali inapoendelea kuweka juhudi Zaidi ya kupunguza bei ya bidhaa hiyo muhimu.

Viongozi wa Kenya Kwanza wanasisitiza ongezeko la bei ya mafuta lipo nje ya uwezo wa serikali na hivyo Wakenya wanapaswa kuvumilia huku serikali ikitafuta mipango kabambe ya kutegua kitendawili hicho.

Akizungumza kwenye hafla ya kupeana msaada wa chakula katika shule ya Msingi ya Kipkaren, kaunti ya Uasin Gishu, Naibu spika wa bunge la Kitaifa Gladys Shollei, aliwarai wananchi kuwa na uelewa kwani kupanda kwa bei ya mafuta imekuwa changamoto ambayo imezidi uwezo wa serikali.

Hii ni changamoto ambayo iko nasi inatukumba na tuelewe kuwa haya yanatokeo tujue kuwa kuna masuala yaliyo nje ya uwezo waw a serikali na hata nje ya uwezo wetu kama viongozi wenu watunga sheria kule Bungeni,” alisemas Shollei.

Hata hivyo, Shollei alisema kuwa serikali imeweka juhudi ya kupunguza bei ya mafuta kwa kutenga fedha ya kupunguza gharama ya bei ya mafuta almaarufu “fuel stabilization fund” na kwa kununua Mafuta kwa makubaliano ya serikali kwa serikali.

Shollei ambaye pia ni mwakilishi wa kike kaunti ya Uasin Gishu alibaini kuwa kuwa iwapo serikali isingeweka juhudi hizo, bei Ya mafuta ingekuwa hata juu zaidi.

Serikali iliweza kutumia kuondolewa kwa ushuru kwa kuweka juhudi za kupunguza bei kwa kutenga hazina ya fedha kupunguza gharama ya mafuta, na pia serikali tutaangalia uwezo wa kuongeza mara mbili zaidi ya hazina hiyo kuimarisha bei za mafuta kwa kutumia mfumo wa ununuzi wa serikali kwa serikali,” alisema Shollei.

Naibu spika huyo alikariri hali hiyo inaweza kubadilishwa iwapo serikali itapunguza uagizaji wa bidhaa nyingi kutoka nje ya nchi haswa mafuta ya kupikia kwa kukuza kampuni za uzalishaji wa mafuta ya kupika hapa nchini.

BY CYNTHIA OCHIENG