AfyaHabariNews

Wadau wa afya waitaka Serikali Ijumuishe Saratani katika Mpango wa Afya kwa Wote, UHC

Washikadau wa maswala ya Afya kaunti ya Kwale sasa wanaitaka Serikali kujumuisha ugonjwa wa Saratani katika mpango wa Afya kwa Wote, Universal Health Coverage (UHC).

Mtaalam wa Ugonjwa wa Saratani ukanda wa Pwani Daktari Riaz Kasmani alitaja  hatua hiyo kua na uwezo wa kupunguza gharama ya matibabu ya saratani kwa wagonjwa wanaolazimika kulipia maelifu ya pesa kwa matibabu hayo.

Akiongea katika Hospitali ya kijamii ya Kinondo, Kasmani alisema kuwa wagonjwa wengi wanataabika kupata matibabu hali inayowapelekea hali inayochangia idadi kubwa yao kupata maafa kwa kukosa kumudu gharama ya matibabu hayo.

Ni muhimu sana katika mpango huu wa Afya kwa wote UHC tunaweza kupata ukaguzi, kujulikana steji ya saratani na kisha matibabu, japo kwa sasa NHIF inashughulikia matibabu kwa kiwango fulani lakini si suala la ukaguzi na mgonjwa anapohitaji kulazwa hilo halijashughlikiwa na NHIF,” alisema Kasmani

Mkurugenzi katika hospitali ya Kijamii ya Kinondo Harrison Kaingu aliiomba serikali kupatia kipaumbele swala hilo. Kulingana na Harrison hatua hiyo itawavutia watu wengi zaidi kufanyiwa uchunguzi ili kupunguza na kutilia pondo vita dhidi ya saratani.

Tungeomba serikali huduma hii ya saratani na kufanyiwa screening ipewe kipaumbele hasa kwenye mradi huo wa UHC ili wengi wafikiwe na wasaidike katika mpango huo, na serikali ikifanya hivi matibabu kupatikana kwa nafuu zaidi wengi hawataumia kama wanavyoumia sasa,” alisema.

Itakumbukwa kuwa Mwezi wa Oktoba ni mwezi wa uhamasiho wa saratani ya matiti kote ulimwenguni.

BY NEWSDESK