HabariNews

Hamasisho Yang’oa Nanga Kukomesha Biashara ya Watoto

Baraza la kitaifa la huduma za watoto  limeanzisha zoezi la kuhamasisha wakaazi wa maeneo mbalimbali nchini kuhusu mpango wa mpito wa watoto walio kwenye vituo vya watoto.

Kwa mujibu wa afisa mkuu wa baraza hilo Abdinur Mohammed, mpango huo unalenga kukomesha biashara ya watoto inayoendelezwa na baadhi ya wamiliki wamaeneo hayo wananoendesha vituo vya kibinafsi.

Akizungumza katika kaunti ya Garissa Mohammed,  alieleza umuhimu wa watoto kulelewa na jamaa zao na katika familia. Kulingana na Mohammed, Aidha tayari mpango huo umekubaliwa katika baadhi ya kaunti huku zoezi la uhamasishaji likiendelea kote nchini.

ili kufanikiha mpango huu kwanza itatulazimu kuwatayarisha wototo kisaikolojizia, kiakili, na pia kuchukua hatua zaidi kufanya uchunguzi wa familia, uwezo wa kifedha na kuona ikiwa familia inuwezo wa kuwaanalia watoto, kwasababu hatuwezi kuchukua watoto na kuwaunganisha na familia bila ya kuchunguza hai ilivyo kwanza.” Alisema

Hata hivyo takwimu za idara hiyo za mwezi Novemba mwaka 2022 zilibaini kuwa zaidi ya watoto 45,000 walikuwa mikononi mwa vituo 885 vya wahisani.

BY EDITORIAL DESK