HabariNews

Tuweni Wakweli! Viongozi Pwani watakiwa Kuilinda Raslimali za Pwani

Kiongozi wa wengi katika bunge la kaunti ya mombasa ambae pia ni mwakilishi wadi wa likoni Athmani Mwamiri amewataka viongozi wa pwani kuwa wakweli kwenye muungano wao wa kulinda rasilimali za pwani na kuzika maslahi yao za kibinafsi na kwa kupigania haki za wapwani.

Akizungumza katika kipindi cha baraza letu Oktoba 21, Mwamiri alisma kuwa iwapo viongozi hao watazika maslahi yao na kutokubali kutumia kisiasa na serikali kuu, muungano huo utachangia pakubwa kulinda bandari ya mombasa ambayo kwa sasa inakisiwa kukodishwa pasi na maoni ya wenyeji na viongiozi kutoka pwani kuhusishwa.

Mwakilishi huyu aidha alisisitiza umuhimu wa kulinda bandari hiyo kwani iwapo bandari hiyo itatolewa mikononi mwa serikali ya ugatuzi kwa asilimia 100 pwani itakoshewa kikatiba na kuachwa maskini kirasilimali.

Mwamiri Kadhalika, alitaja kuwa swala la bandari lisichukuliwe kwa urahisi kwani vijana wengi uwenda wakakosa ajira kutokana msimuo unaokukisiwa na mmiliki mpya ambaye kwa sasa hajulikani.

Hata hivyo baadhi ya wadadisi wanadai kuwa uwepo wa bandari hiyo na hali ilioko kwa sasa inapaswa kuboresha ili kufanikisha ufani wa huduma kazi kitaifa huku wananchi wakidhamiria kuwa viongozi kutoka pwani ndio wakiolegeza kamba na kuchangia hali hiyo.

Haya yanajiri  baada ya viongozi mbali mbali kutoka pwani kuja pamoja wakiongozwa gavana wazamani wa mombasa Ali Hassan Joho kutaka uhusishwaji wa maoni yao kuhusu tetesi za kukodishwa kwa bandari hiyo.

BY DAVID OTIENO