HabariNews

UWAZI Buxton! Wakaazi waendeleza Kilio Cha Mradi wa Nyumba za Kisasa,Mombasa.

Shirika la kutetea haki za kibinadamu la haki yetu kutoka kaunti ya Mombasa limepuzilia mbali madai kuwa linatumika kisiasa katika harakati za kutetea wakazi wa zamani wa buxton kwenye miradi ya ujenzi wa nyumba za kisasa na gharama ya chini.

Akizungumza na Sauti ya Pwani, kipindi cha sauti asubuhi afisa wa mipango wa maswala ya ardhi  katika shirika hilo Munira Ali Omar alisema kuwa madai yao ni ya kupotosha umma ikizingatiwa kuwa Haki Yetu inatekeleza majukumu yake kikatiba.

Utaalamu wetu ni kushughulikia suala la ukosefu wa ardhi na makao katika mkoa wa pwani, na kama haki yetu suala kuu ambalo tutaendelea kulivalia njuga ni kwamba mradi wa nyumba za kisasa Mombasa sio mradi wa kijamii, ni uwekezaji na tutaendele kuliza ni makaazi kwa nani na afueni kwa kina nani?” Alisema.

Munira alimtaka mwekezaji huyo kukoma na kuweka mambo bayana badili ya kuandaa mikutano ya kisiri na baadhi ya wanakamati na wenyeji hao kama ilivyaagizwa na mahakama pamoja na kamati ya seneti iliyoongozwa na senata wa kiambu kimani wamatangi.

Serikali na Yule muwekezaji lazima waache kuwazungusha watu wa Buxton na waitishe mkutano na wtu wote kama ilivyoamrishwa na koti na bunge. Kama kweli huu ni mpango wa kuwapatia watu makao kupitia TPS, waache kuwa na vikao vya siri. Mkutano wa hivi karibuni kati ya mwekezaji na baadhi walioteuliwa haukuwa rasmi hakuna ushahidi hakuna uwazi.” Aliongeza Munira.

Kwa upande wake Naibu katibu mkuu wa wakazi wa zamani na aliyekuwa wenyeji wa buxton John tsuma, mwekezaji huyo alishindwa kueleza ukweli wa mambo badala yake kushirikiana na kamati iliyotupiliwa mbali baada ya wakazi  kuhisi kuwa kamati hiyo inawasaliti kwa kupendelea mipango ya mwekezaji huyo.

TSUMA aidha alishikilia kuwa licha ya makubaliano hayo yote mwekezaji amedinda kuweka mambo bayana hasa kuhusiana mfumo wa tps.

Details mpaka sahii hawajazisema ama kuambia mtu, nyumba haifai kuwa za siri, na tukisema kuwa watu wa Buxton wamekuwa wakwanza kufaidika na mradi wa TPS, ni nyumba zimeuzwa kioff plan, kama lakini ni nyumba anakuja kutupatia hapo sahihi nah ii TPS , nitamkaribisha vizuri sana

BY DAVID OTIENO