Mamlaka ya Baharini nchini,Kenya Maritime Authority iliweweka mkataba wa utendakazi na Kenya Shipping Agency Association ili kutoa nafasi za ajira kwa mabaharia ukanda wa Pwani.
Waziri wa Uchumi Sawamati Salim Mvurya alisema makubaliano hayo ya utendakazi yataimarisha utendakazi wa baharini na kukuza uchumi wa taifa kwa kubuni nafasi za ajira.
Aidha Mvurya alieleza kuwa mkataba huo utatoa nafasi za wawekezaji mbalimbali kuwekeza humu nchini hasa sekta ya bandarini akidokeza kuwa mabaharia watakaomaliza watapata nafasi ya kufanya mazoezi kamili kwa vifaa maalum vilivyopo
“Tumeelewana kufanya pamoja na washikadau mbalimbali,na kila mwanafunzi atakayemaliza atasaidiwa na mafunzo ya majaribio ya kuendesha ndege ili wajue kazi halisi kwa mabaharia wetu”.Asema Mvurya.
Vilevile Mvuya aliwaonya maafisa wanaowahangaisha wavuvi baharini kukoma kuwahangaisha wavuvi hao kwani wanajitafutia riziki ili kujiendeleza kimaisha na kuchangia pakubwa pato la serikali huku akisema mipangilio kabambe itawekwa ili mabaharia hao wapate wawekezaji.
“Sio ruhusu ya kuwangaisha wavuvi ovyoovyo kwani wanajitafutia na jamii zao,ila kama serikali tunaweka mikakati kambambe ili wavuvi wakamilishe mahitaji yanayostahili,hivyo msiwahangaishe wavuvi”.Asisitiza Mvurya.
Kwa upande wake Gavana wa Mombasa Abdulswamard Shariff Nassir aliisifia hatua hiyo ya serikali kuhusisha kikamilifu serikali ya kaunti ili kupanga mipangilio ya bandari kwa umoja.
Aliitaja hatua hiyo itakayowezesha utendakazi mzuri baina ya serikali zote mbili na sekta ya bandari humu nchini.
“Serikali ya kaunti ya Mombasa itasaidia pakubwa na mkutano unaokuja na naimani mpango huu utawezesha kupanua uchumi wa bandari sio Kenya tu bali hata mataifa mengine”.Alisema Abdulswamard Sharrif.