HabariLifestyleNews

Mahakama Kuu yaongeza muda wa agizo la kusitisha maafisa wa polisi kwenda Haiti

Mahakama kuu jijini Nairobi imeongeza muda wa agizo la kuzuia kutumwa kwa maafisa wa polisi nchini Haiti hadi kesi iliyowasilishwa mahakamani itakaposikizwa na kutolewa uamuzi.

Jaji wa Mahakama ya Juu Chacha Mwita ametoa agizo hilo la kusubiri kusikizwa kwa ombi lililowasilishwa na kiongozi wa Thirdway Alliance Kenya Ekuru Aukot na wengine wawili.

Mapema mwezi huu mahakama ilisema walalamishi hao waliibua maswala muhimu ya kitaifa na maslahi ya umma ikumbukwe kuwa Kenya ilikuwa imejitolea kuongoza kikosi cha kimataifa kwenda Haiti kusaidia kukomesha ghasia za magenge ambapo iliahidi kupeleka maafisa wake 1000 kwa oparesheni hiyo.

Ekuru Aukot aliyekuwa mgombea uraisi na mmoja wa walalamishi alisema katiba haikufuatwa kutokana na kutoshirikishwa kwa bunge kabla kuafikiwa kwa uamuzi huo.

Alisema si sheria kutumwa kwa polisi nje ya nchi na kuongeza kuwa atalishtaki baraza la mawaziri kwa kudharau mahakama baada ya wao kuidhinisha kutumwa licha ya agizo la mahakama.

 

By Editorial