HabariNews

KILIO cha Ukosefu wa Hospitali na Wataalsamu wa maradhi ya Akili, Taita Taveta

Wagonjwa wa afya ya akili Ndani ya kaunti ya Taita Taveta wamezidi kutaabika kutokana na ukosefu wa hospitali pamoja na wataalamu wa khudumikia tatizo hilo.

Mapungufu hayo yakichangia wagonjwa katika kaunti hiyo kupelekwa hadi Kaunti nyingine ikiwemo kupokea matibabu ikiwemo Hospitali ya Portreeze iliyoko Mombasa na ile ya Madhare Kaunti ya Nairobi jambo linalotajwa kama changamoto kwa Kaunti hiyo.

Kulingana na David Mgindi mmoja wa vinara katika sekta ya afya , kuna haja ya wizara ya afya Kaunti ya Taita Taveta kufanya kazi kwa karibu na serikali ya kitaifa ili kuimarisha huduma zake na kutoa wito wa kuwepo kwa Hospitali ya kushughulikia tatizo la afya ya akili.

Ukiangalia Taita Taveta na kwengineko, tuko na issues za mental heath ambapo watu wengi kwa sababu ya msongo wa mawazo na mambo mengine kuna tatizo pale. Unapata mtu akiwa na shida lazima apelekwe Mathare Nairobi ama Portriz Mombasa, Tunaomba kuwe na taasisi ndani ya kaunti ambayo inashughulika na mambo kama hayo” Alisema.

Mgindi  hata  hivyo alieleza haja ya Serikali ya Kaunti ya Taita Taveta kujenga Hospitali ya wagonjwa wa afya ya kiakili na kuongeza waatalamu kauntini humo.

BY EDITORIAL DESK