Uncategorized

Asilimia 72.8 ya wakaazi Mombasa wanaridhika na Hudumaza Matibabu

Imebainika kuwa Asilimia 72.8 ya wakazi wa kaunti Mombasa wanaridhika na huduma za matibabu zinazotolewa katika zahanati mbalimbali kaunti hiyo.

Haya ni kwa mujibu wa ripoti ya Utafiti wa TEMA iliyoandaliwa na Shirika la Kuhamasisha Masuala ya uongozi bora, Local Empowerment for Good Governance (LENGGO).

Kwenye utafiti uliofanywa katika ya mwezi Novemba 2022 na Machi 2023 ambapo jumla ya watu 1,604 kaunti hiyo walihusishwa ili kutoa maoni ya kuweka mikakati Bora ya kuimarisha huduma za afya kaunti hiyo.

Aidha ripoti hiyo ilionyesha kuwa kaunti ya Mombasa inakumbwa na changamoto ya uhaba wa dawa.

Mnamo mwaka 2022 na 2023 zaidi ya asilimia 57.7 na asilimia 51.8 ya wakazi wa kaunti hii mtawalia, walisema hawakuwa wakipata dawa za kutosha walipotembelea vituo vya afya huku wengine wakikosa kabisa.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa ripoti hiyo Mkurugenzi wa shirika hilo Lucas Fondo alibaini kuwa ripoti hiyo ni sauti ya mwananchi kulingana na huduma za matibabu anazopata huku akiongeza kuwa ripoti hiyo itawezesha serikali ya kaunti kuboresha huduma za matibabu

Hii ripoti itasaidia serikali kaunti ya Mombasa kufahamu ni mahali gani wanafaa kuboresha huduma zao za afya kulingana na maoni yaliyotolewa na wakaazi.”Alisema Fondo.

Uzinduzi wa ripoti hiyo uliandamana na uzinduzi wa kiunzi (App) ijulikanayo TEMA, mtandao ambao unapigiwa upato kusaidia wananchi kupiga ripoti kuhusu huduma za matibabu kaunti ya Mombasa.

mwananchi wa pale chini kupata hizi huduma kupitia kiunzi ambacho kimezinduliwa leo na kufahamu zaidi kuhusu huduma za matibabu .”Alisema Fondo.

Dkt. Shem Pata Afisa mkuu wa afya kaunti ya Mombasa alisema kuwa uzinduzi wa mtandao huo wa TEMA utawasaidia idara ya afya vilivyo hasaa katika kujua malalamishi na changamoto zinazokumba vituo vya afya katika kaunti hiyo. Alisema idadi kubwa ya vijana imekumbatia mfumo wa teknolojia na mitandao hivyo basi mbinu za awali za kutoa maoni kupitia maadishi katika visanduku vya maoni ilipitwa na wakati.

Wakaazi wa Mombasa hata hivyo walihimiza kutumia mtandao huo wa TEMA kwa manufaa yao.

BY MJOMBA RASHID