Serikali ya kaunti ya Kilifi imewekamikakati yakuziba mianya inyopelekea ogezeko la ufisadi na kutoruhusu malipo ya miradi pasi kupitishwa na kamati za kusimamia miradi mashinani.
Kulingana na Gavana wa Kilifi Gedion Mung’aro, hatua hiyo ni miongoni mwa mbinu ambazo serikali ya Kilifi itatumia kuhakikisha ufisadi unasitishwa, pamoja na kuimarisha uwazi katika utekelezaji wa miradi.
Mung’aro Alisema kuwa serikali imekuwa ikilimbikiziwa madeni ya miradi ambayo haijafanyika jambo lililochangiwa na kutokuwapo kwa njia mwafaka za kuziba mianya ya ufisadi, hatua anayodai kutatiza utendakazi wa serikali ya kaunti hio.
Kwa upande wake mkurugenzi mtendaji wa shirika la KECOSCE Phylis Muema, mashirkia ya kijamii yataendelea kufuatilia utendakazi kazi wa serikali ya kaunti ili kukomesha ufisadi, pamoja na kuhimiza mchakato wa Kushirikisha wananchi kabla ya utekelezwaji wa miradi ili kuongeza uwajibikaji.
Muema Aidha ameonya kuwa endapo serikali itakatisha ushirikiano wake kwa mashirika hayo na wananchi basi watalazimika kuelekea mahakamani.
“Idara ambazo ziko kwa kaunti mara nyingi zilikuwa zinaweka ukuta.sisi tumesema tutawajibika, tutafuatilia bajeti,tutafuatilia ile miradi vile inafanyika na tutaweka ripoti,ikishindikana tunashukuru mahakama iko wazi, tutaweza kujadiliana kuona vile mwananchi anaweza kupata huduma ambazo ziko bora, tutaenda kotini.” Alisema Muemi.