HabariNews

Mombasa yaandaa Mikakati Kabambe wakati wa Likizo Kukuza Utalii kabla ya Ziara ya  Mfalme Charles III

Serikali ya kaunti ya Mombasa imedokeza kuwepo kwa mikakati kabambe ya kuboresha sekta ya utalii hususan msimu wa huu wa sherehe ambapo wanatarajia ongezeko la watalii.

Katika mahojiano ya kipekee na Sauti ya Pwani FM Waziri wa Utalii,Utamaduni na Biashara kaunti ya Mombasa Mohammed Osman alitaja  baadhi ya mbinu wanazopania kutekeleza ili kuhakikisha kuwa watalii wanaowasili sehemu hii wanapokea huduma bora na za kipekee.

Osman alionyesha kuridhishwa kwake na idadi ya watalii wanaozuru kaunti ya Mombasa akibaini kuwepo kwa ongezeko la watalii wanaofika eneo hili kutokana na ndege za kimataifa kutua mjini humo.

Tumehakikisha kwamba tuna mzunguko mmoja wa mfumo wa jumuia ili tusiwe na msimu ya watalii ili hawa watalii wawe na fursa ya kuja kuanzia Januari mpaka Disemba. Tumepigana na serikali kuhusu Hii mambo ya open sky policy kwahio itakua tunapata watalii moja kwa moja kutoka ulaya mpaka kapa hivi. Watalii ambao tulipata mwaka uliopita ni takriban elfu 700 saa hizi tumeongeza adi kufikia Agosti ni watalii elfu 850, ina maana tukifika Disemba tutapita milioni moja.” Alisema

Kulingana na Osman, tayari Mswada wa Kitalii wa Usimamizi wa Fuo za Bahari uliwasilishwa kwenye Bunge la kaunti ya Mombasa ambao utasaidia kudhibiti shughuli za fukwe za bahari na kuzuia maafa pamoja na kuimarisha usalama wa wanaozuru kaunti ya Mombasa kwa jumla.

kuna mswada napitisha unaitwa beach management bill, itasaidia sana kuhakikisha kwamba kuna usalama katia fuo za bahari, kuna security ambao tutaweka , kuna beacha towers, wapiga mbinzi pia kuna vijana ambao tutawaajiri kwa muda wa miezi miwili mitatu kuhakikisha kwamba kuna usalama, atleast tukiendana na shirika la msalaba mwekundu itakuwa tumejiandaa na kuhakikisha kwamba watu wanafurahia likizo zao.”

Vilevile ziara ya Mfalme Charles III na Malkia Camilla katika kaunti ya Mombasa Osman aliitaja kama suala ambalo litaweza kuuza sifa ya Mji wa Mombasa kwa mataifa mengine ulimwenguni kama kivutio cha utalii na kuimarisha sekta hiyo ikizingitiwa kuwa miongoni mwa vikitega uchumi vikuu vya kaunti hii.

Britain ni miongoni mwa watalii wanaozuri Mombasa kwahio itakua wanaongezea ile idadi ya watalii, na mwajua pia akifika (mfalme Charles) atazuru fort jesus na hio itakuwa imeweka katika ramani mji wa Mombasa kuonyesha kwamba mji huo ni miongoni mwa sehemu za utalii ulimwenguni” Alisisitiza

 BY BEBI SHEMAWIA