HabariNews

Tabasamu Pwani, Premier Bank ikizindua Tawi jipwa kwa misingi ya Dini ya Kiislamu

Jamii ya ukanda wa Pwani wana kila sababu ya kutabasamu kufuatia uzinduzi wa Benki mpya inayohudumu kwa misingi na sheria za Kiislamu ijulikanayo Premier Bank.

Akiongea katika kipindi cha Sauti Asubuhi Meneja wa Benki hiyo ukanda wa Pwani Yassir Hydar amesema ujio wa benki ya Premier ni afueni kwa kila Mpwani ambaye amekuwa akisaka huduma za benki zinazozingatia maadili na misingi ya dini.

Alisema takribani matawi 19 ya banki hiyo kote nchini na matawi zaidi ya Matano eneo la Pwani kunatoa fursa kwa benki kuwahudumia wananchi katika masuala ya biashara na uwekezaji.

Wakati uo huo amebaini kuwa wana nia ya kufungua matawi mengine zaidi katika eneo la Pwani ili kukidhi mahitaji wa wakazi na kuwafikia wateja wengi zaidi.

 “Ukiangalia idadi ya watu ambao wangependa kuwa na benki ya Kiislamu ni wengi, hivyo lazima tuweke alama sehemu hizi za Pwani hata Lamu na maeneo ya Pwani Kusini huko ttanue zaidi na kufiisha matawi yetu huko,” alisema.

Wakati uo huo Haidar amebaini kuwa Benki hiyo itajikita zaidi katika suala kidijitali kwa kutumia uvumbuzi wa teknolojia uliopo nchini kurahisisha wateja wake katika miamala na shughuli zao za benki.

Kama ujuavyo siku hizi masuala ya utandawazi na teknolojia imepanuka zaidi. Benki yetu tunataka kutumia majukwaa hayo ya kidijitali, ukitaka kutuma, kuwekeza fedha au kutoa kwenda banki moja hadi nyingine au mteja kwa mteja huduma hizo ziwe mkononi bila kufika kwenye benki yetu,” alisema Bw. Haidar.

By MJOMBA RASHID