HabariMombasaNews

Tahadhari kwa wakazi wa Ziwa La Ng’ombe Mvua ikisababisha Mafuriko

Kuna haja ya wakaazi wa wadi ya Ziwa la Ng’ombe eneo bunge la Nyali kaunti ya Mombasa kushirikiana na kuwa na umoja hasa msimu huu wa mvua kubwa inayoshuhudiwa maeneo mbali mbali hapa Pwani.

Akiziungumza na meza ya habari ya Sauti ya Pwani aliyewania nyadhifa ya uwakilishi wadi eneo hilo Maxwel Khonde alisema kuna haja ya wakaazi kuwa macho na mazingira wanayoishi ili kuzia maafa zaidi.

Khonde aliwataka wakazi kujilinda licha ya eneo hilo kuwa na viongozi akisisitiza kuwa ni jukumu la kila mwanajamii kuwajibika na kujilinda.

Mwito wangu kwa kila mwana ziwa la ngombe ni tuungane sote kwa pamoja tuhakikishe kwamba wakati huu mgumu ambapo mvua inanyesha na maji yaningia katika manyumba tunasaidiana,ukisikia jirani yako anapaza sauti tafadhali kuwa makini kumsikiliza ili tuzuie maafa zaidi. Ziwa la Ngombe it’s our collective responsibility.” Alisema

Wakati huo huo wakazi aidha walipokea tahadhari kuwalinda wanawao dhidhi ya mvua inayokunya maeneo hayo ili kuzuzia athari zozote zinazotokana na mvua. Hadi kufikia sasa hakuna kisa kilichotokea licha ya nyumba za wenyeji eneo hilo kujaa maji.

Wazazi watunze watoto wao kulingana na mafuriko , kulingana na hatari zingine zitakazokuwa zinaletwa na mvua, tunawatahadharisha wakazi wa hapa Mombasa upande wa Ziwa la Ng’ombe kwamba wakae macho. Tuna watahadharisha jamani watuwa Ziwa la Ng’ombe tujichunge sana kwanza ukiona maji yamejaa mahali tunafaa tuangalie sana” Wazazi walisisitiza.

 BY MEDZA MDOE