HabariNews

Benki ya Premiar Yasambaza Matawi yake Pwani, wateja wakihakikishiwa Huduma Bora

Benki ya premiar imeawahakikishia wateja wake kutoka ukanda wa pwani kwamba kuna mikakati dhabiti ya kuhakikisha kuwa wananufaika na  bidhaa zao hasa kwa jamii za kihislamu zinazohitaji huduma za sharia copmlaint .

Akizungumza na meza yetu ya habari wakati wa mkutano na wadau wakuu wa benki hiyo wakiwemo wateja wake, afisa mkuu mtendaji wa benki hio OSMAN DUALLE, aliwahakishia wakazi kutoka ukanda wa pwani kuwa tayari usimamizi wa Premier imeweka matawi kadhaa katika eneo la Malindi Mombasa lamu na Kilifi ili kukidhi mahitaji ya wateja wake.

Eneo la Pwani halijaachwa nyuma katika malengo yetu ya upanuzi, nadi ya mpago wetu tunalenga kufanya upanuzi eneo zima. Tumebainisha maeneo kama Malindi, Mombasa, Lamu na hata Nyali Mombasa, nifuraha yangu kuwajulisha kuwa tawi letu la nyali pale Quick matt litakuwa tayari mwezi ujao.” Alisema Dualle

Kulingana na msimamizi mkuu  wa idara ya kibiashara katika benki hiyo Yahya Dahir, benki imeweka mikakati dhabiti ya kufanikisha usalama wa wateja wao mikononi mwa mamlaka ya almashauri ya KRA na kukiri kwamba Premier inazingatia sheria  na sera za mamlaka hiyo.

Nataka kuwahakikishia kama benki tutafuata sheria za nchi hii, lakini kwa upande mweingine nataka kuwahakikishia kuwa sisi tunahudumu huru mbali na KRA, hakuna akaunti itakayo blokiwa bila ushauri kutoka kwa na hivyo ndivyo tutakavyo jenga uaminifu” Alisisitiza Yahya.

Kulingana na Yahya kuna malengo makuu ya benki hiyo ya kutimiza matakwa ya wateja wake huku akishikilia kuwa premier imekuja kutatua changamoto za kifedha pamoja na kuwajenga wateja wake.

Tunataka kurahisisha biashara za kimataifa kwako, tunataka kukufanyia sahali, tunataka kuhakikisha mtaji tunaotoa kwa biashara ni za Sheria Compliant na kukupatia mkono kifenda sio tu kwa bishara bali hata kwa waajiriwa wako, wamiliki wa biashara muweze kukuza biashara zenu,” Aliongezea.

Duale aliweka wazi malengo ya benki hiyo ikiwa ni kunifanikisha kuleta huduma karibu na wateja wake. Kuhusu usalama wa kimitandao , Osman aliwahakikishia wateja wao usalama wa kutosha na kuondoa hofu wanapofanya biashara na benki hiyo.

BY DAVID OTIENO