HabariNewsUncategorized

Rais Ruto Akutana na Waziri Mkuu wa Czech, Aahidi mazingira mwafaka ya Wawekezaji

Rais Wiliam Ruto amewatoa hofu Wakenya na kuhakikishia Mataifa duniani kwamba Kenya imeweka mikakati na mazingira mwafaka ya kuwavutia wawekezaji.

Kwenye mkutano uliojumuisha Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Czech, Petr Fiala pamoja na wawekezaji zaidi ya 120 katika Ikulu ya Nairobi, Rais Ruto amesema kwamba mazungumzo hayo yataimarisha pakubwa shughuli za ukuaji wa uchumi humu nchini.

Rais Ruto aidha ametoa uhakikisho kuhusu hatua ya maridhiano baina ya Kenya na Czech kwamba yatainua kiwango cha uchumi nchini kwa kuruhusu wawekezaji zaidi.

Ninauhakika kua taifa la Kenya na Jamuhuri ya Czech zitashuhudia harakati kuu za kibiashara zitakazostawisha ongezeko la uwekezaji kutoka kwa kampuni za Czech Nchini Kenya katika sekta mbali mbali katika uchumi wa taifa. Hii itakua Uamuzi wa kimikakati baina ya mataifa haya mawili” Alisema Rais

Kenya na Jamhuri ya Czech zimeahidi kuimarisha uhusiano wao na kutumia fursa zilizopo za uwekezaji katika nchi hizo mbili.

Rais Ruto amesema hivi karibuni nchi hizo mbili zitatia saini makubaliano ya kiuchumi yaliyojadiliwa ambayo yatawezesha Kenya kupata masoko yasiyo na ushuru na vikwazo.

Haya yanajiri huku ikiarifiwa kwamba wawekezaji zaidi elfu 6 wamejiondoa katika soko la hisa ya Nairobi na huku mamia ya wawekezaji wengine wakiripoti kuhamia Mataifa mengine.

BY MJOMBA RASHID