HabariNews

Kuvuja kwa paa la JKIA ni Utepetevu wa Wanakandarasi wa Serikali iliyopita! Asema Waziri Murkomen

Wanakandarasi waliokabidhiwa kazi ya kukarabati Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta, JKIA wameagizwa kufanya marekebisho haraka iwekazakanavyo kufuatia baadhi ya sehemu kwenye angatua hiyo kuvuja mvua.

Akizungumza na waandishi wa habari huko Diani alipokagua uwanja wa ndege eneo hilo Waziri wa Uchukuzi Kipchumba Murkomen amelalamikia hatua ya shughuli za ukarabati katika angatua nyingi nchini zimedudumaa suala analolitaja kudororesha hadhi ya sehemu hizo na kutatiza shughuli za usafiri.

Murkomen alilalamikia hali hiyo akitaja kuwa kuvuja kwa mapaa ya angatua ya JKIA ni kutokana na utendakazi duni wa wanakandarasi na wahandisi waliokuwa wakifanya ukarabati wakati wa uongozi wa rais mstaafu Uhuru Kenyatta.

Waziri huyo aidha alidai kuwa wanajandarasi hao waliharakisha ukarabati huo pasi kuzingatia ubora wa viwango waliyowekewa kwa kuwa serikali hiyo iliyokuwa mamlakani ilikuwa katika harakati ya kusimamia mradi wa ukarabati.

Tayari nimeongea na wale contractors walifanya kazi hiyo na wahandisi walisimamia kazi hiyo na tumekubaliana na wale wasimamizi lazima warudie wafanye kazi ile vizuri, kwa kuwa haikufika ile kiwango inahitajika kwa mambo ya projetcs ndio unaona JKIA tuko na shida ya stima, nilijaribu kusuluhisha mambo ya jenereta juzi bado tulipata giza,” alisema.

Murkomen aidha aliwataka wanakandarasi waliokabidhiwa majukumu ya kukarabati upya uwanja huo kituo cha 1C na 1E kutekeleza wajibu wao ipasavyo.

Vilevile  waziri huyo amedokeza baadhi ya mikakati wanayopania kutekeleza ili kuimarisha shughuli za usafiri katika angatua ya kimataifa ya jkia ikiwemo kuweka mitambo mbadala ya kusambaza nguvu za umeme.

Nimewaambia wafanye mabadiliko zaidi na yule contractor ashaweka jenereta lakini anaenda polepole amesingizia kwamba akienda mwendo wa kasi ingehariobu network zingine za stima airport. Nimesema hata kama ni kuongeza ma contractors wengine lazia tutafute uwezo zaidi ili kuhakakikisha tunamaliza suala la stima once and for all, interchange ya jenereta iwe automatic sekunde 30 ndio tumekubali,” alisema Murkomen.

Kauli ya Murkomen inajiri huku seneta wa Nandi samson Cheragei akimsuta vikali waziri huyo akisema hajaimakinikia wizara anayoiongoza ipasavyo.

BY MJOMBA RASHID