HabariMichezoNewsSports

Mchezo wa Bao Ukuzwe, Viongozi Kilifi wapaza Sauti zao Kukuza Michezo ya Kitamaduni

Mchezo wa kiasili wa bao maarufu Kigogo ni miongoni mwa michezo iliyokosa kupewa kipaombele licha ya kutambulisha utamaduni wa taifa la Kenya. Baadhi wanaendele kujizatiti kuweka mchezo huu katika ramani na kuona kwamba unatambulika kimataifa.

Mchezo huu ambao unawachezaji zaidi ya elfu 30 kote ukanda wa pwani, unatajwa kuwa miongoni mwa michezo ya asili iliyotumika kuunganisha  jamii ila jambo na kusikitisha ni kuwa mchezo huo haujapewa kipaumbele ikilinganishwa na michezo mingine.

Kulingana na Ray Katana Mwaro diwani wa Sokoni kaunti ya Kilifi, mikakati ya kuboresha na kuutangaza mchezo huo iling’oa naga kwa kuandaa ligi, itakayoshirikisha wachezaji na vilabu vyote katika kaunti ya Kilifi na ukanda wa pwani kwa jumla. Alisema watahakikisha kuwa serikali ya kaunti ya Kilifi inatenga mgao maalum utakao saidia kustawisha mchezo wa bao.

Wajipange watengeneze mfumo wa ligi vile atachezwa kauti yote tuweze kupeleka injili ya kigogo kaunti nzima, alafu ligi iwe inachezwa, sisi kazi yetu na mweshimiwa wa baya kayzi yetu tutatafuta pesa tutaziweka pale tuhakikishe mchezo wa kigogo unaeleweka” Alisema Mwaro

Diwani wa Gongoni Stephen Baya Mwaro kwa upande wake, talanta za mchezo huo zinapotea kwa kukosa uwekezaji mzuri na badala yake kuangazia michezo mingine ya kigeni.

Mwaro aliisihi serikali kuruhusu hamasa ya mchezo huo kufanyika sehemu mbali mbali ikiwemo taasisi za masomo, ili mchezo huo uweze kutambulika katika ngazi za kimataifa na kuwasaidia wachezaji kunufaika na mchezo huo kama vile wachezaji wanaoshiriki michezo mingi.

watu wengi wameangazia sana talanta zile za kigeni kwa mfano mipira, na hapa chini tuko na michezo yetu ambayo ni ya kitamaduni na imesahauliwa mfano Bao iko tu wanaicheza vijijini na inaishia vijijini. Sahii nataka kutumia nguvu yangu na nafasi yaku na hata kuitengea pesa ili kwamba tukaweze kuinua ili ikishajulikana hawa nao wataanza kufaidika. Tutakua tunauza hii michezo yetu itajulikana nawatu wetu wa hapa hapa na hata itajulikana mpaka nje” Aliongezea Baya

BY ERICKSON KADZEHA