HabariNews

Mafuta ni Yangu! Mfanyabiashara Anne asisitiza; aeleza aliyoyapitia alipotoweka

Mfanyabiashara Anne Njeri Njoroge aliyekuwa ameripotiwa kutoweka amebaini kuwa alichukuliwa na maafisa wa Idara ya upelelezi punde tu alipomaliza kuandikisha taarifa.

Mfanyabiashara huyo alidai kuwa alifika katika makao makuu ya DCI Nairobi kulalamikia kuwa mafuta yake aliyoagiza yalikuwa hatarini kuibwa.

Kulingana na Njeri, alilazimika kuandikisha taarifa baada ya kukutana na waziri wa kawi Davis Chirichir aliyemweleza kuwa mafuta hayo hayakuwa yake bali ya kampuni ya Galana Energies na Aramco.

Kulingana na vile niliambiwa nika apply kwa EPPRA na after that nilikuwa nikisubiri kupewa import permit ambayo sikujua inahitajika,”

Na wakati nikusibiri nilienda kumuona CS Chirchir na akanimbia mafuta sio yangu tena ni ya kampuni inajiita Galana nikamwambia sijauza mafuta yangu wala sija sign na kampuni hiyo kwa hivo mafuta ni yangu ndio akasema haiwezekani ni nifanye kuenda kwa CID Headquarters kurekodi statement na nikafanya vile na after kumaliza ndio ilikuwa wakati wangu wa kutoweka,”

Akizungumza na wanahabari nje ya majengo ya Mahakama ya Mombasa alikofika kufuatilia kesi hiyo, Njeri alieleza masaibu aliyokutana nayo mikononi mwa maafisa waliomkamata baada ya kuandikisha taarifa.

Niliambiwa twende ofisi nyingine tuandikishe statement nyingine, lakini kufika chini nilipata sio ofisi, ni mtu alikuwa akiitwa Karanya na Yuris ambao waliniambia kama nilikuwa na dawa natumia. Wakati walinichukua kwa gari niliambiwa nipatiane simu na password, na nikawapatia sababu nafuata sheria,” alisimulia.

Nkiwauliza mnanipeleka wapi na ni usiku na mbona mmenitenganisha na wale tulikuwa na wao wakaniambai nitulie tu nifuate sheria, kisha wakanifunga macho.”

Nikaomba sasa kuwamabia tafadhali msiniue mimi ni mama niko na watoto wananihitaji nina familia wananihitaji, naomba msimwage damu yangu sijakula cha mtu wala sijaiba ila tu nimeleta mafuta sielewi ya kwamba nimetolewa DCI office,” aliongeza.

Njeri alieleza alivyofungiwa katika chumba kimoja na hata kutishiwa maisha kabla ya kuachiliwa baada ya maafisa hao kubaini ukweli wake.

Nilienda nikilia Mwenyezi Mungu msiniue mimi ni mama, wakati tulifika pale nikaambiwa nishuke sijui ni wapi nikiwa bado nimefungwa uso, nikaingizwa ndani nikiwa nimeshikiliwa nikaingia ndani ya chumba ina matress na chain ya kufungiwa kapelekwa kufungiwa nikaambiwa natakikana niseme ukweli sababu nisiposema ukweli sitaona watoto wangu tena.” Alisema Bi. Anne.

Kwa upande wake Bi Anne akiwa kifungoni kwa muda wa siku hizo alipewa chakula cha kutosha lakini alikataa katakata kula chakula hicho na badala yake akiitisha kahawa tu akihofia kuwa chakula hicho kilikuwa na sumu.

Niliogopa kukula kile chakula mwanzo sababu nilifikiria chakula kina sumu ama si kizuri,” alisema.

Anne alifika kortini akiandamana na wakili wake Cliff Ombeta huku kiini cha kesi yake kikiwa ni umiliki wa tani 93,000 za dizeli ambazo pia zilidaiwa na kampuni mbili ambazo ni kampuni ya Galana Energies na ile ya Aramco.

Wakili Ombeta hata hivyo aliishtumu serikali kwa kumnyanyasa na kumhangaisha mteja wake akidai kuwa serikali iliyachukua mafuta yake mfanyabiashara huyo kwa njia ya ulaghai.

Acha niwaambie serikali iko na uhusiano na haya mafuta ni Serikali imeyachukua. Serikali imeiba haya mafuta kwa sababu hayakuwa yao lakini wameingiza kwenye pipeline yao, huo si ni wizi na wanadai karatasi zake ni ghushi. Huu ni unyama na ukatili huwezi kumchukua mtu na kumfungia siku nne na kumfunga na minyororo kwa chumba hakuna choo na kumzuia kwenda choo ni shida lazima aombe ruhusa na saa zingine akiomba ruhusa wanakataa kuja,” alisema Ombeta.

Haya yanajiri siku moja tu baada ya Wasimamizi wa Mamlaka ya Bandari, KPA kumshutumu mwanabiashara huyo kwa kudai kuwa alighushi nyaraka alizotumia kudai umiliki wa shehena hiyo.

BY MJOMBA RASHID

Comment here