Habari

Watatu Wafariki, familia 3800 Zikithirika kutokana na Mvua Kali Mombasa

Watu 3 wamethibitishwa kufariki huku takribani familia 3,800 kaunti ya Mombasa zikithirika kutokana na mvua kubwa iliyoshuhudiwa maeneo ya Pwani.

Akizungumza na wanahabari gavana wa kaunti hiyo Abdul Swamad Sharrif Nassir aliwahisi wakaazi wanaoishi maeneo ya karibu na bahari kuweza kuhamia maeneo salama akidokeza utabiri wa hali ya anga umeonyesha uwezekano wa mvua hiyo kuendelea.

Gavana Nassir aliyakanusha madai ya kuwa mafuriko hayo ni kutokana na hali mbaya ya mabomba ya maji taka.

Hesabu zetu zaonyesha kuwa familia 3,800 zimeweza kuathirika na watu 3 wamepoteza maisha yao 2 wao wakiwa wakaazi wa ambao walikuwa wanaishi karibu na bahari na mwengine alipigwa na shoti baada ya kukanyaga nyaya za umeme.”Alisema Gavana

Wakati huo huo gavana alielezea ushirikiano na asasi mbali ikiwemo shirika la msalaba mwekundu huku akiongeza kuwa hospitali tatu ikiwemo hospitali ya rufaa pwani maarufu ‘Makadara’ zitaongezewa mda wa kuhudumu ili kutoa huduma zozote za dharura.

Kulinagana na Nassir maeneo yaliyoathirika zaidi ni Bamburi ,Utange pamoja na Bombolulu.

Serikali ya kaunti ya Mombasa tumeweza kuweka mikati ya kusaidia zile familia zilizoathirika tutafanya kazi pamoja na Redcross ,tunashukuru usaidizi kutoka kwa UNICEF na Jamii Buhora kwa kutoa mabomba ya kutoa maji.” Aliongeza gavana

Katibu katika idara ya kuangazia maeneo Kame na maendeleo ya kimikoa Kello Harsama, hata hivyo aliwahakikishia waathiriwa katika kaunti ya Mombasa kwamba serikali imetoa magunia 560 ya mchele, 560 maharage katoni 200 za nyama ya kusagwa magodoro 300, blanketi500 miongoni mwa bidhaa muhimu za jikoni kusadia waathiriwa hao.

Harsama alisema kwamba msaada huo utagawanywa kuanzia jumapili hii huku akiahidi msaada zaidi kuletwa na serikali kuu kusaidia waathiriwa hao kikiwemo chakula na bidhaa nyengine muhimu.

BY NEWS DESK