HabariNews

Hamasisho la kwa Washikadau Barabarani kukabili Ongezeko la Ajani Nchini

Visa vya ajali za Barabarani vimeripotiwa kuongezeka nchini huku uendeshaji wa kasi ya juu na utumizi wa vileo kwa madereva vikitajwa kuwa sababu kuu za ajali hizo.

Akizungumza na wanahabari katika hafla ya kutoa hamasa kwa Madereva hapa Mombasa Afisa Mkuu wa Bodi ya Wahandisi nchini EBK Margaret Ogai alisema hatua ya kuongezeka kwa ajali hizo ni kutokana na madereva kukaidi sheria na kanuni za Barabarani.

Ogai aliwataka madereva kuwa makini na kuzingatia masuala yanayofaa pamoja na kutimiza mahitaji stahiki ili kuhakikisha usalama wao pamoja na wateja wao.

Aliwahimiza vile vile wananchi kuchukua jukumu la kuwawajibisha madereva barabarani iwapo hawatozingatia maadili stahiki kwa kususia kuabiri magari yao ili kujilinda dhidi ya maafa yoyote.

Kwa upande wake Mkuu wa Chama cha Madereva na Makanga kaunti ya Mombasa Khalifa Mwatsahu aliwataka madereva kutopuuza sheria na kanuni za barabarani huku akisisitiza haja ya madereva kupewa mafunzo zaidi ili kudhibiti visa vya ajali za barabarani.

Mwatsahu hata hivyo aliwahimiza wamiliki wa vyombo vya usafiri kuhakikisha madereva wanaowaajiri wameafiki vigezo stahiki ikiwemo kuwa na vibali vya kuendesha ili kuepuka kujipata katika mkono hatari ya sheria.

Hafla hiyo iliyoandaliwa na Bodi ya Wahandisi nchini (EBK) kuadhimisha Siku ya kuwakumbuka Waathiriwa wa Ajali za Barabarani pamoja na kutoa hamasa na mafunzo stahiki kwa madereva ili kuepuka maafa katika siku za usoni.

BY BEBI SHEMAWIA