HabariNews

KILIFI YATAJWA KIELELEZO BORA NCHINI, ULIMWENGUNI UKIADHIMISHA SIKU YA CHOO

Kaunti ya Kilifi imetajwa kuwa kielelezo bora katika juhudi zake za kuwahamasisha wakazi kudumisha usafi kwa kujenga vyoo ili kutunza mazingira na kujikinga na maradhi humu nchini, ulimwengu ukiadhimisha siku ya choo

Kwenye hafla ya kuadhimisha siku ya choo ulimwenguni, juhudi za kaunti ya Kilifi kuhakikisha kuwa wakazi wake wanakoma kujisaidia mwituni zilitambuliwa na kupelekea kaunti nyingine ikiwemo Siaya, Kitui, Migori na Busia kutafuta mafunzo zaidi kutoka kwa kaunti ya Kilifi.

Akiongea kwa niaba ya waziri wa afya kaunti ya Kilifi Clara Chonga, alisema kuwa kaunti hio imepiga hatua kubwa ukilinganisha na takwimu zilizotolewa mnamo mwaka 2019 zilizoonesha kuwa kati ya nyumba 100, 17 kati yake hazina sehemu za kujisaidia na kuiweka kaunti ya Kilifi miongoni mwa kaunti 15 zilizokuwa na wananchi wengi wanaojisaidia mwituni ila kwa sasa idadi hiyo imepunguwa kwa kiwango kikubwa.

Eneo bunge la Kilifi kusini lilitajwa kufaulu kwa asilimia 100 kwenye kampeni hiyo ya kuhamasisha wakazi kudumisha usafi kwa kuchimba vyoo kaunti ya Kilifi.

Kwa upande wake naibu gavana Florence Mbetsa Chibule, wito umetolewa kwa wakazi kuendeleza juhudi hizo ili kujiepusha kuathirika na mkurupuko wa maradhi.

Alielezea kuwa asilimia 60 ya visa vya magonjwa katika hospitali zote kaunti ya Kilifi hutokana na ukosefu wa kudumisha usafi.

….

Maadhimisho hayo yenye kauli mbiu kuongeza kasi ya mabadiliko kwa kufanya chochote unachoweza ili kudumisha usafi humu nchini, yalifanyika katika kijiji cha Mwembe Kati eneo bunge la Kilifi kusini.

BY ERICKSON KADZEHA