Wizara ya madini na uchumi samawati imeahidi kuwekeza kwa ujenzi wa bandari ya wavuvi na uwekezaji humu nchini.
Akizungumza wakati wa kuadhimisha siku ya wavuvi duniani eneo bunge la Likoni kaunti ya Mombasa waziri wa madini Salim Mvurya alidhihirisha kuwa mkataba wa kwanza wa ujenzi wa bandari hizo tayari ushawekwa sahihi na utagaharimu takriban shilingi Bilioni 1.5. Shilinigi bilioni 2.6 zikihitajika kwa ujenzi wa bandari ndogo kwenye sehemu tofauti ikiwemo Mombasa,Lamu na Ziwa Victoria.
“Tushaweka saini mkataba wa kwanza sasa katibu anatengeneza bajeti na itagharimu bilioni 1.5,tunaangalia kama Bilioni 2.6 amabayo tutaweza kujenga bandari za wavuvi na hizi ni zile bandari ndogo.” Alisema Mvurya.
Wakati huo huo Mvurya alidokeza kuwa hivi karibuni watazindua mpango wa kutathmini idadi ya samaki inayopatikana katika sehemu flani (Stock Assesment) na mpangilio maalum wa kupata viumbe mbali mbali baharini (Marine Spartial Plan)
Mvurya aliamrisha mashirika yanayohusika na usafi wa mazingira kuhakikisha yanahusisha kikamilifu makundi mbali mbali ya wavuvi (BMU’S)
“kwanza tutaanzisha zoezi la Stock Assesment lazima tujue samaki wako hapa ni wangapi badae tutafanya zozezi lingine la Marine Spartial Plan tujue katika hii bahari tunaweza kupanga vipi kamba wanapatika zaidi,shemu hii ni samaki hawa.” Aliongeza Mvurya.
Kwa upande wake Gavana wa kaunti ya Mombasa Abdul Swamad Sharrif Nassir aliwarai viongozi mbali mbali humu nchini kushirikiana na kufanya kazi kwa umoja kama njia moja ya kustawisha taifa.
Kulingana na Nassir ni sharti wizara zote zishirikiana na serikali za kaunti badala ya kujitenga ili kuimarisha uchumi wa taifa huku akipongeza Wizara ya uchumi samawati kwa kushirikiana na washidadau mbali mbali kwenye sekta ya uvuvi akiitaja hatua hiyo kama moja itakayoimarisha sekta hiyo.
“Nawapatia kongole wizara ya uchumi samawati na pengine itakuwa ni funzo kwa wizara nyingine waweze kujua ya kuwa hawawezi kufanya kazi bila ushirikiano lazima washirikiane na serikali za kaunti. “Alisema Nassir.
Wakati huo huo gavana Nassir aliwarai wabunge wa kaunti na tume ya mgao wa mapato kuhakisha wanatetea ugatuzi na kuhakikisha wanapigania ardhi ya bahari kwa wavuvi humu nchini.
“Ikiwa tunaweza kukubali kuwa ugao wa ardhi usiwe ni ardhi ya kukanyaga pekeyake lakini mpaka ya bahari kwa sababu ndani pale kuna raslimali ambayo serikali imeekea wizara nzima na kutoka na hili tutakuw ana njia ya kushindana na ndugu wenye kusema sisi tunamiliki pakubwa.”Alisema Nassir.
Haya yamejiri huku Kenya ikijumuika na mataifa mengine duniani kuadhimisha Siku ya Wavuvi Ulimwenguni kauli mbiu ya mwkaa huu ikiwa ni kujenga mazingira bora kwa wavuvi na kuwezesha wavuvi wadogo wadogo.