HabariLifestyleMazingiraPhotography

Serikali imehimizwa kukumbatia upanzi wa mmea wa rangi maarufu (Bixa) ili kukuza na kuwaendeleza wakulima wa mmea huo hapa nchini.

Kulingana na Mwenyekiti wa Mamlaka ya Kilimo na uzalishaji wa chakula (AFA) Cornelly Serem alisema kuna haja ya serikali kuacha kuagiza mmea wa rangi kutoka mataifa ya nje badala yake kuwasaidia wakulima kukuza mmea huo hapa nchini.

Aidha Serem aliahidi kufanya kila awezalo ili kuhakikisha wakulima wa mmea huo wanaangaziwa kikamilifu ikiwemo kupewa mafunzo ya kukuza mmea huo.

“Hatutaendelea kuagiza mmea rangi kutoka mataifa ya nje ikiwa tunajua wazi kwamba kuna mmea wa BIXA ukanda wa Pwani,imefikia wakati wa kuwasaidia wakulima wetu humu nchini kwa kununua mmea rangi ili kuwasaidia kupata karo badala ya kutegemea mataifa mengine na tukifanya hivi tutakuwa tunapiga hatua nzuri zaidi”.Alisema Serem.

Kwa upande mkurugenzi wa kilimo biashara Chrobart Muthee Mwoga alidokeza kuwa mmea huo utasaidia kukuza uchumi wa taifa kwa kutoa ajira kwa vijana huku akiwahimiza wakulima kutia bidii katika upanzi wa mmea huo.

“Zaidi ya asilimia 40 ya watu humu nchini imekumbatia mmea huu na inasaidia katika usalama wa chakula,kusaidia katika zao la taifa ambapo pia vijana wengi watapata ajira huku tukipunguza garama ya maisha”.Alisisitiza Muthee.

Kwa upande Kiongozi wa chama cha kuwaunganisha na kuwatetea wakulima Francis Kianga alisema ni sharti wakulima wajumuishwe kikamilifu na maswala yao yaangaziwe ikiwemo kulinda sheria za wakulima kutokana na kulaghaiwa na mawakala.

“Seikali za kaunti na serikali kuu zishirikiane na kujumuisha mkulima vilivyo hususan maswala ya vyeti ili wakulima wasilagaiwe na mabadali katika sekta hii na ndio maana tumekuja hapa ili kuangalia sheria zitakazisaidia mkulima katika mmea huu”.Alisema Francis.

Hatua hiyo ilijiri baada ya mamlaka hiyo kuwahusisha washikadau mbalimbali na wakulima ili kupitia mapendekezo ya sheria za mmea huo ili kushinikiza serikali kuungazia kikamilifu mmea huo ambapo Cornelly Serem aliwaongoza washikadau pamoja na wakulima kuzindua rasmi kitabu kilichokuwa na mapendekezo ya sheria za mmea huo.

MWISHO.