Wanandoa katika Jamii ya waislamu nchini walitakiwa kukumbatia uvumilivu katika ndoa badala ya kukimbilia talaka za kila wakati.
Kulingana na Kadhi mkuu nchini Sheikh Abdulhalim Athman alisema kuvunjika kwa ndoa kumeacha watoto wengi kuhangaika kwa kukosa malezi bora kutoka kwa wazazi.
Kulingana na kiongozi huyo ni jukumu la wanandoa kupendana kuheshimiana na kuvumiliana pamoja na kutafuta ushauri kwa wazazi na viongozi wa kidini ili kuishi vyema kwenye ndoa zao.
“Ningependa kusisistia kuhusu jambo la kufanya suluhu ambalo ni jambo muhimu na vilevile ni hitajio la kikatiba.Serikali yenyewe inapendekeza suala hili,”alisema Kadhi mkuu.
Wakati huo huo Kadhi alisisitiza tasisi za mafunzo ya kidini ya kiislamu na washauri wa maswala ya ndoa kuingilia kati ili kusaidia waumini kwa ushauri nasaha mwafaka wa kukabiliana na changamoto ya ndoa dhidi ya kuvunjika.
“hapa Mombasa kuna taasiis amabazo zinashughulikia mabambo ya kupatanisha wanandoa.Tunaomba vitu va masomo viweze kuongeza mafunzo ya kindoa kaama miongoni mwa kozi ambayo itafundishwa kwa watu ili wapate mafunzo kuhusiana na masuala ya ndoa.” Kadhi aliongeza.