Shirika la wanyamapori KWS inaendeleza mchakato wa kumsaka simba anayedaiwa kumuuwa mhudumu wa bodaboda eneo la Marere.
Akizungumza huko Kwale afisa msimamizi wa mbuga ya wanyamapori eneo la Shimba Hills Chonga Steven alisema maafisa wa shirika hilo bado wanendelea kumtafuta simba huyo .
“ Kulingana na uchunguzi na matukio yake kuonekana, simba ni huyo mmoja na simba huyu ni wa kuja .” Alisema Chonga
Wakati huo huo Chonga aliwashauri watumizi wa barabara ya Kwale kuelekea Kinango kuchukua tahadhari zaidi na kutumia vyombo vya usafiri salama.
“ Pale ni ndani ya mbuga, leo kuna simba ndovu pia wako pale ndani na wanyama hawatabiriki, kuna nyai pale ndani pia wanaweza vamia. Sisi tunasema kama watu pale wawendani ya magari, wakiwa ndani ya magari wako salama lakini hizi mbinu zengine huwa zinatatiza wale wanyama,” Aliongezea
Haya yanajiri kufuatia kisa cha mwili wa mwanamume mmoja kupatikana ukiwa umeshambuliwa maeneo ya Kwale. Jamaa huyo anadaiwa kushambuliwa na simba akiendesha piki piki.