HabariNews

Afueni! KCB yatoa ufadhili wa Sh. 800M, Wanafunzi 20 Wakifaidika Mombasa

Ni afueni kwa takribani wanafunzi 20 kutoka kaunti ya Mombasa baada ya kupata ufadhili wa masomo ya shule ya upili kutoka kwa wakfu wa benki ya KCB.

Kulingana na mkurugenzi wa wakfu huo tawi la Kilindini Collins Obiero, wanashirikiana na serikali ya kaunti hiyo kuhakikisha linaipa kipaumbele swala la elimu hasa kwa wanafunzi wanaotoka kwenye familia maskini.

Obiero alidokeza kuwa katika ufadhili huo benki ya KCB imetenga shilingi 800,000,000 kote nchini huku akiongeza kuwa idadi ya wanafunzi waliotuma maombi imeongeza mwaka huu ikilinganishwa na miaka ya nyuma.

Kama KCB tumekua na ushirikiano na sekta ya elimu kwa muda na tunaweka azma kama benki kuweza kuwashika mkono hawa wasomi 20 ambao waekusanyika hapa leo kuwasaidia wanapoendelea na masomo.

Katika huu  mradii benki imetoa shilingi 800M kote nchini

Katibu wa kaunti hiyo anayesimamia utumishi wa umma Jeizan Faruk alihimiza wazazi kuwasaidia watoto wao kupata elimu huku akiwashauri wanafunzi waliopata ufadhili huo kutilia manani masomo yao.

Tumehimiza wazazi kuendelea kuwasaidia watoto wao kukamimilisha masomo yao vile vile wanafunzi kuchukulia furasa hii kuwa ya muhimu,tumekuwa na miradhi sawia na hio iliyozinduliwa na gavana wiki jana ambapo tunanuwia kusaidia shule za mchana kwa takribani kima cha shilingi 100m na zile za malazi kwa shilingi 100m kaunti ya Mombasa” Alisema Faruk

Kwa upande wao wazazi na wanafunzi wamepongeza ufadhili wakisema utawawezesha kutimiza ndoto zao.

Ninashukuru KCB kwa fursa hii kuwasaidia watoto wasiojiweza ,sisi kama wazazi tuna furaha.” ” Ninafuraha kwa fursa hii itaniwezesha kutimiza ndoto zangu.” Alisema Mzazi

BY MEDZA MDOE