HabariNews

40 Zake Zatimia! Wakazi wamwua Mshukiwa wa wizi huko Lunga Lunga

Mshukiwa mmoja wa wizi ameuawa katika kijiji cha Kalalani, eneobunge la Lungalunga kaunti ya Kwale baada ya kudaiwa kuiba pikipiki.

Waendeshaji bodaboda na wakazi wenye ghadhabu wamemkamata mshukiwa huyo na kumpa kipigo cha mbwa koko kabla ya kumwua kwa kuchoma moto.

Inadaiwa kuwa mshukiwa huyo kwa jina Nyale Nyawa aliiba pikipiki aina ya Boxer kutoka kijiji Jirani, pikipiki ambayo ilifuatiliwa na kupatikana nyumbani kwake.

Inaarifiwa kuwa mmiliki wa Pikipiki hiyo Mkala Greza aliwasilisha ripoti kwa kampuni aliyonunua pikipiki hiyo ambayo ilifuatiliwa na kupatikana nyumbani kwa mshukiwa huyo.

Kulingana na Kamanda wa Polisi eneo la Lungalunga mshukiwa huyo wa umri wa miaka 38 aidha anasemakana kuwa na kesi ya unajisi wa mtoto wa 14 iliyoripotiwa katika kituo cha Lungalunga.

Polisi pia waliwanusuru wasichana wawili wenye umri 14 na 17 katika nyumba ya mshukiwa huyo ambao wanasemekana kuolewa naye.

Pikipiki hiyo kwa sasa inazuiliwa katika Kituo cha polisi cha Lungalunga huku uchunguzi kuhusiana na tukio hilo ukianzishwa.

BY OUR REPORTER