HabariNews

Afua ya Utalii Mombasa! Ndege zaidi za Kimataifa kutua Mombasa

Sekta ya Utalii kaunti ya Mombasa inatarajiwa kuimarika zaidi kufuatia mashirika zaidi ya ndege za Kimataifa kuazimia kuanza safari za moja kwa moja hadi mjini humu.

Waziri wa Utalii na biashara kaunti ya Mombasa, Osman Mohamed alielezea matumaini ya utalii kuimarika maradufu hasa kutokana na uwepo wa mfumo wa anga huru (open-sky policy).

Alisema hatua hiyo imefungua mwanya kwa ndege zaidi kuiga mfano wa shirika la ndege la Fly Dubai lenye safari za moja kwa moja kutoka Dubai hadi Mombasa.

“Kuna ndege nyingi ambazo tunatarajia zije kama hii ya Fyl Dubai ni kampuni kutoka Eldoret zitakuja mara nne kwa wiki hapa Mombasa na ndege moja inabeba asilimia 170 na juzi tulikuwa na kikao na waziri wa uchukuzi na tukabuliana kwamba ndege kama ATP Airlines ndizo tunajarajia ziweze kutua hapa Mombasa.” Alisema Osman

Wakati huo huo waziri Osman alisema kaunti ya Mombasa imebuni mikakati zaidi kuvutia watalii mbali mbali kupitia bahari na makavazi kama njia ya kubuni ajira.

BY JAPHET MAKANAKI