HabariNews

Wito wa Utu, Stretchers lakataa Usambazaji wa Picha za Waliouwawa

Wito umetolewa kwa watumizi wa mitandao kutosamabaza picha za watu waliouliwa kinyama au kihalifu bila kuficha utambulisho wao.

Shirika la Stretchers Youth Organisation la maswala ya vijana lilisema hatua hiyo huenda ikasababisha familia za waathiriwa hao kuwa na msongo wa mawazo pamoja na dhiki.

Katika taarifa kwa vyombo vya habari Shirika hilo liliwarai watengenezaji wa maaudhui mitandaoni kuwa makini wanapofanya maudhui ya kujulisha watu kuhusu mauaji ya wanawake likisema watenegenezaji wa maudhui mitandaoni wanajukumu kubwa la kufahamisha na kubadilisha mawazo ya jamii kuhusu dhulma za kijinsia.

Shirika hilo liliitaka serikali kuchukua jukumu la kuchunguza visa vya mauaji ya kinyama ya wanawake na kuhakikisha waliohusika na mauaji hayo mwanakabiliwa na mkono wa sheria .

Haya yanajiri huku kukiwa na msururu wa ripoti za jamii ya kike kuuwawa kikatili wengi wao wakiwa wasichana kutoka maeneo mbali mbali nchini Kenya.

BY NEWS DESK