HabariNews

EACC yawanasa Maafisa 9 wa KPA kwa Ulaghai wa Zabuni

Watu 9 wakiwemo maafisa wa Halmashauri ya Bandari nchini KPA wanafikishwa mahakamani kujibu mashtaka ya ufisadi dhidi yao.

Kulingana na Tume ya maadili ya Kupambana na ufisadi nchini, EACC tisa hao wanakabiliwa na tuhuma za ufisadi wa kima cha shilingi milioni 62.

EACC imesema kuwa Baadhi ya washukiwa hao walikamatwa jana katika bandari ya Mombasa na wengine mapema leo.

Akithibitisha kukamatwa kwa watu hao, Msemaji wa EACC Erick Ngumbi amebaini kuwa 6 kati ya waliokamatwa ni maafisa wakuu wa KPA na wengine ni wanakandarasi wa kibinafsi.

Tisa hao wanafikishwa mahakamani Mombasa kushtakiwa kwa makosa mbalimbali yakiwemo kughushi stakabadhi za kandarasi ili kupata zabuni na ulaghai wa zabuni miongoni mwa mashtaka mengine.

Haya hapa majina ya maafisa hao tisa waliokamatwa:

  1. Yobesh Oyaro – Aliyekuwa Mkuu wa Idara ya Ununuzi na Ugavi, KPA
  2. David Angwenyi – Mwanachama wa Kamati ya Tathmini, KPA
  3. Norah Mugambi – Mwanachama wa Kamati ya Tathmini, KPA
  4. Athanase Wambari -Mwanachama wa Kamati ya Tathmini, KPA
  5. Robert Bosuben – Afisa Mwandamizi katika Idara ya Uhandisi wa Ujenzi, KPA
  6. David Arika – Mwanachama wa Kamati ya Tathmini, KPA
  7. Azenath Kwamboka Mageto – Wakala wa Chemiso East Africa
  8. Rose Cherotich – Mtia saini wa Chemiso East Africa.
  9. Idd Arube Nanyang – Wakala wa Chemiso East Africa

BY MJOMBA RASHID