Rais William Ruto amewaonya walimu wakuu wa shule dhidi ya kuwarejesha nyumbani wanafunzi kutokana na ukosefu wa karo.
Akizungumza huko kaunti ya Meru wakati wa uzinduzi wa nyumba za bei nafuu, rais alibaini kuwa serikali yake ilisambaza shilingi bilioni 62 mwezi huu pekee kwenye shule mbalimbali akikariri kuwa wakuu hao hawana sababu ya kuwarejesha wanafunzi nyumbani.
Rais Ruto alisema kuwa fedha hizo zilisambazwa katika shule zote za msingi na sekondari pamjona na vyuo vya kiufundi na kwamba wakuu wa shule hawapaswi kuwahangaisha wanafunzi.
“ kama serikli ya Kenya tumetoa pesa kwa mwezi huu pekeyake wa Januari , tumetoa billion 62 ya kusomesha watoto. Hakuna mzazi ataulizwa pesa shuleni ati kwa sababu serikali imechelewa” Alisisitiza
Wakati huo huo katika utendakazi wa serikali katika sekta ya elimu, rais Ruto alisifia serikali yake kwa kufanikisha kuajiriwa walimu wengi zaidi ndani ya mwaka mmoja pekee.
Kiongozi huyo wa nchi aidha aliahidi kupelekwa mswada bungeni ili kuajiriwa walimu elfu 20 zaidi ili kuimarisha sekta hiyo.
“Mwaka ulioita tuliajiri walimu ellfu 56 wa kusomesha watoto wetu. Mwaka huu tena, mimi napeleka mapendekezo bunge tuajiri walimu wengine elfu 20, kwasababu tunataka mtoto wa maskini na tajiri wapate nafasi sawa ya kusoma shuleni na mtoto asiende shule akose mwalimu” Aliongezea rais.